ACT WAZALENGO YAITAKA SERIKALI KUPITIA UPYA MFUMO WA TAASISI ZA MIKOPO NCHINI - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 7 March 2023

ACT WAZALENGO YAITAKA SERIKALI KUPITIA UPYA MFUMO WA TAASISI ZA MIKOPO NCHINI

 Share

Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Tanzania Bara Dorothy Samu  ambaye
pia ni Waziri Mkuu Kivuli akizungumza leo wakati wa Kongamano la
Kitaifa
la Wanawake wa ACT lililofanyika Jijini Tanga ambapo alisema mikopo hiyo
badala
ya kuwa mkombozi kwa wanawake imekuwa mizigo kwao.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Tanzania Bara Dorothy Samu ambaye
pia ni Waziri Mkuu Kivuli akizungumza leo wakati wa Kongamano la
Kitaifa la Wanawake wa ACT lililofanyika Jijini Tanga ambapo alisema
mikopo hiyo badala ya kuwa mkombozi kwa wanawake imekuwa mizigo kwao.
aziri Kivuli wa Wizara ya Wanawake,Watoto na Makundi Maalumu Janeth Rite akizungumza wakati wa kongamano hilo
Na Mwandishi Wetu,TANGA

Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Tanzania Bara Dorothy Samu ameitaka
Serikali kupitia upya mfumo  mzima wa Taasisi zisizo
za Kiserikali zinazotoa mikopo na kuangalia riba zao kutokana na kuwa zimekuwa
mzigo kwa wanawake na kupelekea kushindwa kurejesha na wakati mwengine kukimbia familia zao

Dorothy
ambaye pia ni Waziri Mkuu Kivuli aliyasema hayo leo wakati wa Kongamano la Kitaifa
la Wanawake wa ACT lililofanyika Jijini Tanga ambapo alisema mikopo hiyo badala
ya kuwa mkombozi kwa wanawake imekuwa mizigo kwao.

Alisema kwa
lazima Serikali iangalie kwa umakini riba ambazo zimetolewa na taasisi hizo ambayo
sio himilivu na sio rafiki kwa wanawake ambao ndio wakopaji wakubwa katika
kuendeleza biashara zao za ujasiriamali.

“katika hili
tunaitaka Serikali kuangalia kwa umakini taasisi za mikopo ambazo zimekuwa riba
kubwa na kupelekea kushindwa kurejesha na kukimbia familia zao hili ni tatizo
liangalie hasa ile inayoitwa Kausha Damu “Alisema

- Advertisement -

Awali
akizungumza Waziri Kivuli wa Wizara ya Wanawake,Watoto na Makundi Maalumu Janeth
Rite aliitaka Serikali kuhakikisha Halamshaueri zinakuwa na uwiono sawa katika
utoaji wa fedha za mikopo asilimia 10 zinazotokana na mapato ya ndani.

Alisema kwa sababu
hali ilivyo hivi sasa imekuwa ikiwabagua baadhi ya wananachi kutokana na
itikadi ya vyama vyao jambo ambalo sio nzuri kwa ustawi wa maendeleo hapa
nchini.

“Suala hilo
la mikopo zinazotoka kwenye Halmashauri lazima kuwepo na usawa pamoja na
kuondosha upendeleo ambao umekuwa ukipelekea manunguniko kwa wanawake kutokana
na itikadi zao za kiasiasa”Alisema

Waziri huyo
alisema kwamba kwa mujibu wa takwimu zilizopo ni asilimia 80 ya wanawake wapo kwenye
 sekta ya kilimo ambao wanalima kwa
kutumia jembe kilimo ambacho hakina tija kwao kutokana na kupata mazao hafifu.

Alisema kwa
sababu hakina tija ndio maana Chama hicho katika mipango tyao watakapo pata
ridhaa ya kuongoza nchi watawaondoa kwenye ujasiriamali usiokuwa na tija
ikiwemo kuwapeleka wenye tija ambao wanaweza kukopesheka.

- Advertisement -

“lakini pia
Serikali iweze kuona namna nzuri ya kutoa mikopo kwa wakina mama ili waweze
kuongeza wigo mpana wa uzalishaji mazao ya chakula ndipo itapoondosha  changamoto zao za kiuchumi “Alisema

Hata hivyo
alisema wakina mama wakiendelea kutumia jemnbe la mkono wasahau mafanikio yao
kupitia sekta ya kilimo kutokana na kwamba kuna haja ya kubadilika kwa kulima
kisasa.

No comments:

Post a Comment