BARAZA LA CHUO MZUMBE LAANZA KAZI KWA KUTEMBELEA MIRADI - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 1 March 2023

BARAZA LA CHUO MZUMBE LAANZA KAZI KWA KUTEMBELEA MIRADI

 


Wajumbe wa Baraza walipowasili katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo na kupokelewa na wenyeji wao, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha na Naibu wake anayeshughulikia Fedha na Utawala,  Prof.Allen Mushi.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof.Mwegoha (kushoto), akiwaongoza Wajumbe wa  Baraza kutembelea hosteli za Maekani. Kulia kwake ni Mjumbewa Baraza,  Bi. Suzane Ndomba.

- Advertisement -

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof.William Mwegoha, akiwaonesha Wajumbe wa Baraza ramani ya eneo la ujenzi Maekani iliyotokana na na Mpango Bora wa Matumizi ya Ardhi ulioidhinishwa na Baraza (Master Plan).

Wajumbe wa Baraza wakipokea maelezo kutoka kwa Prof. William Mwegoha (Mwenye Suti), kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi Maekani.

- Advertisement -

Wajumbe wa Baraza wakiwa wakipokea maelezo ya awali kuhusu utendaji wa Kituo cha Afya Mzumbe, kinachotoa huduma za afya kwa wafanyakazi, Wanafunzi  na wananchi wa vijiji jirani, walipotembelea kituo hicho wakati wa ziara yao ya kukagua miradi na shughuli za chuo.

Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Saida Yahya-Othman (katikati), baada ya kumaliza kikao cha kwanza cha utambulisho kilichofanyika Makao Makuu ya Chuo, Morogoro.

- Advertisement -

……………………

Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, walioteuliwa hivi karibuni na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, wamekutana kwa mara ya kwanza katika kikao cha maalumu cha 124, kilichofanyika Kampasi Kuu Morogoro, Jumanne tarehe 28 Februari 2023, kikiongozwa na Mwenyekiti Prof.  Saida Yahya- Othman.

Akiwakaribisha katika kikao hicho, Prof. Saida ameeleza furaha yake ya kupata wajumbe wa Baraza, na kuwaahidi ushirikiano katika kutekeleza malengo ya Baraza hilo katika kusimamia utendaji wa Chuo, ambao utazingatia kanuni, taratibu, sheria na miongozo iliyopo katika kuhakikisha Baraza linafanya kazi zake kwa weledi.  

Amewaahidi ushirikiano katika kipindi chote cha uongozi wake, huku akiwataka kuwa huru kkuchangia na kuleta mawazo mapya ambayo yatafanya Chuo kiweze kusonga mbele kitaaluma.

Akiwakaribisha wajumbe hao kwa niaba ya Menejimenti, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha, amewapongeza na kuwakaribisha wajumbe hao Chuo Kikuu Mzumbe, na kueleza kwa undani shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Chuo hicho katika kutoa elimu, Utafiti, Ushauri wa Kitaalamu na Huduma za Jamii, huku akiwahakikishia ushirikiano katika kuhakikisha kwa pamoja Chuo Kikuu Mzumbe, kinapiga hatua kimaendeleo.

Pamoja na kikao hicho, wajumbe walipata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na chuo hicho eneo la Maekani yakiwemo mabweni ya wanafunzi na jengo la madarasa lililokamilika, ujenzi wa eneo la mahafali na jengo jipya la utawala, pamoja na kutembelea Kituo cha Afya na Jengo la Utawala.  

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here