Wednesday, 22 March 2023
FREIGHT MANAGEMENT YAJA NA MPANGO KUBORESHA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI NCHINI
Meneja Operation wa Freight Management Ltd, Dorine Gibson akifafanua jambo wakati wa semina fupi ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Kampuni hiyo mbinu za kisasa za kuboresha huduma wa usafirishaji nchini.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI inayotoa huduma za anga za ugavi na usafirishaji nchini, Freight Management Company Ltd (FMCL), imetangaza mpango wake mpya wa kutoa huduma bora za anga za ugavi na usafirishaji kama sehemu ya mchango wake katika kukuza uchumi wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FMCL Witness Panga amesema wantaka huduma za anga za ugavi na usafirishaji ziwe kwenye kiwango bora ndani ya nchi na kimataifa.
Akirejea jitihada na marekebisho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi, Witness amesema kampuni yake imejipanga vizuri kusaidia mipango ya Serikali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwenye ugavi na usafirishaji na huduma zingine nchini Tanzania.
Alielezea huduma za ugavi na usafirishaji kama nguzo muhimu katika kuchechemua ukuaji wa biashara na uwekezaji na hivyo kukuza uchumi wa taifa na kuleta maendeleo kwa watanzania.
“Matokeo chanya katika uchumi wetu yatainua na kuboresha hali ya maisha ya Watanzania wa kawaida,” amesema na kuongeza kwamba: “Kwa vile sisi ni sehemu ya jamii hii, mchango wetu kwa maendeleo haya ni muhimu na haukwepeki.”
Amesema kampuni yake ina wabia wenye mtandao mkubwa na ulioimarika, unaoiruhusu kampuni kutoa huduma zinazoaminika na zenye gharama nafuu kwa wateja wake (wa ndani na kimataifa).
Pamoja na huduma zingine, kampuni ya FMCL inatoa huduma za anga za ugavi na usafirishaji, ambazo ni pamoja na usafirishaji wa mizigo kwa njia ya anga, usafirishaji wa kuunganisha kwa njia ya anga, kubadili meli/kuhamisha shehena na huduma za kukodisha.
“Tunatoa huduma mbalimbali za ugavi na usafirishaji baharini, ikiwa ni pamoja na usafiri wa kuunganisha kwa njia ya anga, kubadili meli/kuhamisha shehena na huduma za kukodisha, ukaguzi wa mizigo na kutoa hati ya utakaso wa ushuru,” amesema.
Kampuni inatoa pia huduma za ushauri na uchanganuzi. “Wafanyakazi wetu wana uzoefu wa kuweza kutoa suluhisho lililo bora zaidi kwa mchororo wa mahitaji ya ugavi na usafirishaji.”
Katika kufanya kazi zake, Freight Management inatoa huduma za usafirishaji wa kimataifa kwa njia ya anga na baharini kutoka huduma za usafirishaji wa kawaida hadi huduma changamani.
Kimsingi, FMCL ina uwezo wa kutoa huduma yoyote ya usafirishaji, kutoka vifurushi vidogo hadi makontena makubwa. Wafanyakazi wetu wazoefu wanajituma kuhakikisha shehena za wateja wetu zinafika muda wake, salama na ndani ya bajeti.
“Tunajivunia pia huduma ya usafirishaji wa mizigo baina ya nchi na nchi, tukitoa kwa wateja wetu fursa za uchaguzi wa njia ya kutumia, kwa viwango nafuu zaidi na kwa huduma bora.
Huduma za utaratibu wa ugavi na usafirishaji ni pamoja na utakaso wa ushuru, kufunga mizigo, kuhifadhi mizigo ghalani, usambazaji, usimamizi wa orodha/hesabu ya vitu/bidhaa na usafirishaji.
No comments:
Post a Comment