HALMASHAURI YA CHAMWINO YAJIVUNIA MAFANIKIO YA AWAMU YA SITA,RC SENYAMULE AIPONGEZA - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 7 March 2023

HALMASHAURI YA CHAMWINO YAJIVUNIA MAFANIKIO YA AWAMU YA SITA,RC SENYAMULE AIPONGEZA

 Share

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 7,2023 jijini Dodoma katika Mwendelezo wa Programu maalumu ya kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ndani ya kipindi cha miaka miwili katika Halmashauri ya Chamwino Dodoma .

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Chamwino Dkt. Semistatus Mashimba, akizungumza wakati wa kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ndani ya kipindi cha miaka miwili katika Halmashauri ya Chamwino Mkoani Dodoma

- Advertisement -

Na Mwandishi wetu-DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,ameelezea mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita katika kipindi cha miaka miwili ndani ya Wilaya ya Chamwino kwa kujivunia miradi inayotekelezwa Chamwino

Hayo ameyasema leo Machi 7,2023 jijini Dodoma katika mwendelezo wa kutangaza mafanikio ya Serikali kwa Taasisi za Umma zilizopo Mkoani hapa vinavyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mhe. Senyamule ametaja miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa na Serikali katika Wilaya hiyo;
“Tunafahamu pia ujenzi wa Ikulu katika Wilaya ya Chamwino upo katika hatua za mwisho, Dodoma ndio makao Makuu hivyo miradi yote ya kimkakati iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.”amesema RC Senyamule
Pia amesema kuwa Kuna Hospitali yetu ya Uhuru ambayo nayo kwa kiasi kikubwa inatoa huduma kwa wakazi wanaozunguka eneo hilo, zote hizi ni jitihada za serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha sekta za Afya, Miundombinu, Elimu na Ustawi wa Jamii.
Kubwa katika wilaya hii ni ujenzi wa Bwawa la Membe, Chamwino – linalogharimu shilingi Bilioni 10.9, lenye uwezo wa kutunza maji lita 12 Bilioni na kumwagilia Ekari 8000 kwa Mwaka. Haya ni mapinduzi makubwa katika kilimo yanayoenda kuleta uhakika wa chakula kwa wana Dodoma” Amesema Mhe. Senyamule.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Chamwino Dkt. Semistatus Mashimba,  ameelezea mafanikio ya Serikali kwenye uboreshaji wa Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya katika kipindi cha miaka miwili;
“Tumefaniwa kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwa ni mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka miwili kama vile kuanzishwa kwa ujenzi wa vituo viwili vya afya (Itiso na Manda) na Zahanati 4 (Mlazo, Mazengo, Chiwona na Wilunze). Jumla ya Zahanati 2 (Manchali B na Mzula zimeanza kutoa huduma” Amesema Dkt. Mashimba
Kadhalika, Serikali imefanikisha usimikwaji na uanzishwaji wa huduma za mionzi katika Hospitali ya Uhuru, kuanzishwa kwa huduma za upasuaji katika Hospitali ya Wilaya na jumla ya kina mama 89 wamefanyiwa huduma hiyo.
 
Kwa upande wa ukusanyaji wa mapato ya ndani, Halmashauri inajivunia kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato tangu kuanzishwa kwa mfumo wa kieleketroniki wa ukusanyaji wa mapato Serikalini “LGRCIS” ambao umeweza kurahisisha utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara pamoja na kuwezesha utunzaji wa kumbukumbu za biashara.
 Aidha, uboreshaji wa miundombinu ya biashara umewezesha kukua kwa sekta ya biashara na kuvutia wafanyabiashara kufanya biashara katika Halmashauri.
Mkurugenzi huyo pia ameongelea mafanikio katika sekta ya kilimo;
“Kwa upande wa sekta ya kilimo, Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko kwenye sekta hii kwa kufufua shamba la Chinangali lililoanzishwa mwaka 2009 kwa kuliwekea miundombinu miundombinu mipya ya umwagiliaji pamoja na kupanua shamba kutoka ekari 300 hadi kufikia ekari 1000. Pia Serikali imetenga bajeti ya kujenga kiwanda cha kusindika zabibu ili kuondoa kero ya soko la zabibu. Eneo la kujenga kiwanda lenye jumla ya ekari 17 limeandaliwa na utekelezaji utaanza ndani ya mwaka huu wa fedha.” Dkt. Mashimba

No comments:

Post a Comment