KANISA HALISI KURINDIMA SIKU NANE VIWANJA VYA TEGETA NYUKI, IKIFANYA MKUTANO WA 'WIKI YA UKOMBOZI WA MAISHA YAKO', NI KUANZIA JUMAPILI HII - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Thursday, 2 March 2023

KANISA HALISI KURINDIMA SIKU NANE VIWANJA VYA TEGETA NYUKI, IKIFANYA MKUTANO WA 'WIKI YA UKOMBOZI WA MAISHA YAKO', NI KUANZIA JUMAPILI HII


Hayawi hayawi, yamekuwa! Kanisa Halisi la Mungu Baba, kuanzia Jumapili hii, Machi 5 hadi Machi 12, 2023 au 5 Adari hadi 12 Adari Majira Moja Halisi, 'litakiwasha' kwa kufanya Mkutano mkubwa wa Ibada kwa siku nane mfululizo katika Viwanja vya wazi, eneo la Tegeta Nyuki, Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo utafanyika ikiwa ni wa kwanza Kanisa hilo kufanya mikutano ya Ibada zake katika viwanja vya wazi kwa kuwa tangu kuanzishwa kwake hapa nchini takriban miaka mitano sasa, limekuwa likifanyia mikutano ya Ibada zake hadi mikoani, lakini  katika nyumba za Ibada au viwanja vya soka.

Kutokana na hali hiyo Mkutano huo unatarajiwa kuwavutia watu wengi hasa wale wenye kumtafuta au kumjua Mungu wa kweli (Chanzo Halisi), hivyo bila shaka kutakuwa na patashika ambayo pengine itabaki kuwa historia kwa watakaofika au kuutazama mubashara kwenye vyombo vya habari.

Akitangaza Mkutano huo Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga, Dar es Salaam, Jumapili iliyopita, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi, alisema Mkutano huo ni wa Ibada ya 'Wiki ya Ukombozi wa Maisha yako' kwa kuzingatia  Isaya 35:10.

"Kwa zaidi ya wiki moja tutakuwa pale, ni wakati wa kupeleka 'Sauti' kila mahali, maana hatutakiwi kumuweka Mungu mfukoni, lazima tumuweke wazi watu wote wamjue, na baada ya pale Nyuki tutaenda kwingine ambako tutajua baadaye.

Mnajua kuna watu huwa wanasema wanatukubali, lakini hawaelewi yale tunayofanya, wengine wakituona na maji hata huwa hawajui yana maana gani, sasa tunataka siku hizo tutakazokuwa pale wajue, na kila mwenye haki atakayefika pale kama alikuwa na majanga yaliyokuwa yanamuandama, yote yatafutika", akasema Baba Halisi.

Alisema, kila siku, Mkutano wa Ibada hiyo utakuwa unaanza saa 9 alasiri hadi saa 11 jioni, hivyo akawaomba watu wote bila kubagua dhehebu au dini zao kufika kwa kuwa Kanisa Halisi halibagui yeyote maana watu wote ni wa Mungu.

Pia aliwakumbusha Uzao (Waumini wa Kanisa hilo), kwenda na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kufanya uzalishaji, akiwakumbusha kwamba Ibada ni Uzalishaji kwa hiyo kwenda kuuza bidhaa kwenye Mkutano wa Ibada hoyo itakuwa ni pia kukoleza Ibada yenyewe.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi

No comments:

Post a Comment