KANISA HALISI LAANZA KWA KISHINDO MKUTANO WA IBADA YA 'WIKI YA UKOMBOZI WA MAISHA YAKO', KATIKA VIWANJA VYA TEGETA NYUKI, DAR, LEO - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 7 March 2023

KANISA HALISI LAANZA KWA KISHINDO MKUTANO WA IBADA YA 'WIKI YA UKOMBOZI WA MAISHA YAKO', KATIKA VIWANJA VYA TEGETA NYUKI, DAR, LEO

 Kanisa Halisi la Mungu Baba, leo Jumapili hii, Machi 5, 2013 (Adari 5 Majira Moja Halisi), limefanya kwa kishindo Mkutano wake wa kwanza wa Ibada ya kumpeleka Mungu kwenye Umma, uliofanyika katika Viwanja vya wazi, eneo la Tegeta Nyuki, Jijini dar es Salaam.


Mkutano huo umeweza kutia fora licha ya kwamba ni wa kwanza kwa Kanisa hilo kufanya mikutano ya Ibada zake katika viwanja vya wazi kwa kuwa tangu kuanzishwa kwake hapa nchini takriban miaka mitano sasa, limekuwa likifanyia mikutano ya Ibada zake hadi mikoani, lakini  katika nyumba za Ibada au viwanja vya soka.

Akizungumza kwenye Ibada hiyo, Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Baba Halisi amesema Mkutano wa Ibada hiyo utaendelea kufanyika mfululizo kwa Siku nane kwenye Viwanja hivyo vya Tegeta Nyuki na kuwataka wakazi wa eneo hilo kufika kila siku ili wapate baraka na kufutiwa mabaya kama kuibiwa, kurogwa na kudhulumiwa mali zao.

"Ukifika katika Mkutano huu, ukawa ni mwenye haki, basi ujue hutakutana na bahati mbaya, kusingiziwa, mikosi, kuibiwa au kupoteza poteza hovyo mali zako, maana Chanzo Halisi atafuta yote kwako, na kama ulikuwa huwezi kujenga, utajenga, kama biashara yako ilikuwa inayumba basi itanyooka na hata kama familia yako ilikuwa inayumba itatulia.

Baada ya kufika hapa hata kama ulikuwa umekata tamaa ya kuishi, hali hiyo itafutika na utakuwa mwenye furaha katika kila jambo lako, hutatamani tena kujinyonga.

Basi kwa kuwa tumelea baraka hapa Tegeta nyuki, tumeileta kwa ajili ya kila mtu, usikose kufika, wala usihofu mavazi haya meupe, njoo tu na vazi lolote, vazi hili jeupe ni unavaa ukiwa unajua maana yake", akasema Baba Halisi.

"Basi baada ya kusema hayo, leo nimefanya ufunguzi tu, katika mikutano ya kuanzia kesho na kuendelea watakuwepo wahubiri wengi tu ambao wataaachia baraka za Chanzo Halisi hapa. basi tufanye shukurani kisha nitazunguka uwanja huu kuachia baraka", akasema Baba Halisi kisha akaanza kuzunguka Uwanja wote wa mkutano huo akinyunyiza damu safi nyeupe (maji).

Baada ya kujerea jukwaani alifanya tena shukurani (maombi) ya baraka ya mkutano huo na kuwabariki wote waliohudhuria kisha akaaaga na kuondoka akiwaombea wote kila la kheri.

Kiongozi Mkuu wa kanisa Halisi na Mungu Baba lenye Makao yake Makuu Tegeta Namanga, Dar es Salaam, Baba Halisi akitoa mahubiri katika Mkutano wa Nje wa Kumpeleka Chanzo Halisi (Mungu) kwa Umma, uliofanyika katika Viwanja vya Tegeta Nyuki, leo jioni.

Zifuatazo ni picha zaidi za mkutano huo👇

Baba Halisi akifanya shukurani kuubariki mkutano huo wakati ukianza.
Uzao wakipokea shukurani wakati Baba Halisi akifanya shukurani ya kubariki mkutano huo.
"Mkutano huu ni kwa ajili ya kuachia baraka za Chanzo Halisi kwenu ninyi wakazi wa hapa Tegeta Nyuki, njooni mzichote baraka hizi, wala msiogope mavazi haya meupe, njoo tu na vazi lolote, vazi hili unavaa ukijua maana yake..", akasema Baba Halisi.
Uzao (waumini) na wasio waumini wa kanisa Halisi wakajaa wakimsikiliza Baba Halisi kwenye mkutano huo.
Baadhi ya waliohudhuria mkutano huo wakawa wanawauliza baadhi ya uzao, ili kujua Kanisa Halisi ni kina nani hasa? hapa huyu mama wa Kimasai akawa anapewa majibu na uzao.
Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste la Kariakoo, Kanyaro Razaro akisoma bango linaloonyesha uumbaji hatua kwa hatua hadi kufikia majira Halisi, alipokuwa kwenya mkutano huo.
Kisha Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste la Kariakoo, Kanyaro Razaro akapata maelezo kutoka kwa Mtekeleza Sauti kuhusu Majira Halisi na Uumbaji.
Mtekeleza Sauti akiwaeleza jambo vijana kuhusu Kanisa halisi kwenye mkutano huo.
Uzao akiwa na mtoto wake, wakati akimsikiliza Baba Halisi.
Mara huyu kijana akaanguka, bila shaka baada ya kuingiwa na maneno ya Mungu kutoka kwa Baba Halisi, ikabidi asaidiwe kuinuka.
Baba Halisi akazunguka uwanja wote kuachia baraka kwa wote waliofika na ambao hawakufika kwenye mkutano huo. Halafu ikafuatia patashika nguo kuchanika, waliohudhuria mkutano huo wakiserebuka wakati Bendi ya nyimbo za kumuinua Mungu wakipiga wimbo 'Wewe ni Mwema'👇







Mwanamuziki King Maluu, akinogesha wimbo huo
-------------------
Kisha Baba Halisi akafanya shukurani kuwatakia kila la heri waliohudhuria na ambao hawakuhudhuria mkutano huo, halafu akaaga.
Baba Halisi akisindikizwa na Mnara Mmoja Halisi wakati akishuka kutoka jukwaani, tayari kwa kuondoka eneo la Mkutano.
Baba Halisi akipanda gari lake tayari kwa kuondoka baada ya Mkutano huo ambao kesho utaendelea tena katika Viwanja hivyo vya Tegeta Nyuki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here