Rais wa Kenya William Ruto na kiongozi wa Upinzani Raila Odinga wameungana katika ukosoaji wao wa uamuzi wa mahakama ya juu zaidi wa wiki jana ambao unaoruhusu jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja kusajili Vikundi vya harakati zao nchini Kenya.
Rais Ruto sasa ameapa kuwa kamwe hataruhusu ndoa za watu wa jinsia moja nchini Kenya, ambapo alisema 'inakwenda kinyume na tamaduni na imani za kidini za nchi hiyo'.
Haya ni maoni ya punde zaidi ya kiongozi wa ngazi za juu kuhusu uamuzi huo, ambao wengi wametafsiri kimakosa na kudhani kuwa inaipa jamii ya wapenzi wa jinsia moja nchini humo uhuru wa kufunga ndoa.
Ijumaa iliyopita Mahakama ya Juu iliamua kwamba uamuzi wa bodi ya asasi zisizo za serikali nchini Kenya kukataa kuandikishwa kwa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja au kikundi kingine chochote chenye maneno 'mapenzi ya jinsia ndani yake, ulikuwa kinyume cha sheria.
Mahakama ilikuwa imesema kuwa kunyima kundi hilo kusajiliwa kwa misingi ya jinsia zao ni ukiukaji wa haki zao za kikatiba za kujumuika na uhuru wa kutobaguliwa.
Hata hivyo tangu wakati huo, kumekuwa na hasira kutoka kwa umma, bunge, jumuiya ya kidini, viongozi wenye nguvu za dola akiwemo Spika wa bunge la taifa, na sasa Rais mwenyewe.
Jana bunge lilijadili hukumu hiyo kwa kirefu, na wajumbe wengi waliozungumza walishangaa kwa nini mahakama hiyo ilitoa uamuzi wa kutoa uhuru wa kujumuika kwa kile walichoeleza kuwa ni kinyume cha sheria.
Katiba ya Kenya inaruhusu ndoa kati ya watu wa jinsia tofauti pekee, huku kanuni ya adhabu inaadhibu ngono ‘kinyume na utaratibu wa asili’ kwa kifungo cha hadi miaka 14 jela.
Haya ndiyo masharti ambayo wabunge wa Kenya wamekosoa uamuzi huo. Leo, naibu wa Rais Rigathi Gachagua alisema kusajili kikundi kinachopigania haki za wapenzi wa jinsia moja kufunga ndoa ni jaribio la kuhalalisha vitendo vya LGBTQ nchini Kenya ambavyo ‘vilikuwa chukizo kwa haki na mtindo wetu wa maisha’.
Rais William Ruto- kwa shangwe kutoka kwa umati - alipendekeza kulikuwa na kampeni ya wageni kuanzisha 'mazoea ya kigeni' nchini, ambayo aliapa kutoiruhusu Kenya.
Naye Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga pia amenukuliwa akisema kuwa haikuwa jukumu la idara ya mahakama kutunga sheria.
Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa ukosoaji dhidi ya wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya na kanda nzima ya Afrika mashariki, huku mamia ya machapisho ya mitandao ya kijamii yakizuia majaribio yoyote ya kusawazisha mjadala huo.
Siku ya hukumu, mbunge wa Kenya Peter Kaluma aliwasilisha notisi rasmi akitaka kufanyia marekebisho sheria ya kuwapa kifungo cha maisha watu waliopatikana na hatia ya ulawiti au kuikuza.
Nchini Uganda, baadhi ya wabunge pia wanataka kuwasilisha tena mswada wa kupinga LGBTQ wenye adhabu kali kwa ngono ya wapenzi wa jinsia moja au. Mahakama ya kikatiba ya Uganda ilibatilisha mswada huo mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment