Kocha wa Manchester United Erik ten Hag anataka kusajili angalau wachezaji wawili muhimu msimu huu wa joto, huku mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, na kiungo mshambuliaji wa Ajax Mghana Mohammed Kudus, 22, akiwa miongoni mwa malengo yake.(Manchester Evening News).
Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, pia anasalia kulengwa na Manchester United msimu huu wa joto. (Sport - kwa Kihispania)
Manchester City wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic msimu huu wa joto, wakati mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 atakuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake Chelsea. (Telegraph - usajili unahitajika)
Beki wa Chelsea na Muingereza Ben Chilwell, 26, ni mchezaji mwingine anayelengwa na Manchester City msimu ujao. (Football Insider)
Mshambulizi wa Athletico Paranaense raia wa Brazil Vitor Roque anasema yuko tayari kujiunga na Barcelona, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 kunyatiwa na Arsenal. (Sport, kupitia Express)
Klabu ya Borussia Dortmund na klabu ya zamani ya Naby Keita ya RB Leipzig zina nia ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Guinea, 28, mkataba wake wa Liverpool utakapokamilika msimu huu. (Bild - kwa Kijerumani)
Atletico Madrid wamekubaliana na beki wa Uturuki Caglar Soyuncu, 26, juu ya uhamisho wa bila malipo mkataba wake Leicester City utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (90 Min)
Walengwa wakuu wa Real Madrid msimu huu wa joto ni Bellingham na beki wa RB Leipzig wa Croatia Josko Gvardiol, 21. (Sport - kwa Kihispania).
N'Golo Kante alikuwa na chaguo la kuondoka Chelsea kwa uhamisho wa bila malipo msimu huu lakini kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 31, anataka kusalia Stamford Bridge na anakaribia kuafikia mkataba mpya. (Fabrizio Romano)
No comments:
Post a Comment