YANGA SC YATANGULIZA MGUU MMOJA FAINALI CAFCC - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 10 May 2023

YANGA SC YATANGULIZA MGUU MMOJA FAINALI CAFCC

 

WAWAKILISHI Pekee katika Kombe la Shirikisho barani Afrika Timu ya Yanga SC imejiweka nafasi nzuri ya kutinga Fainali ya Michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya nchini Afrika Kusini katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa  nusu fainali uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha kwanza timu zote zilikuwa zikishambualiana kwa zamu na kupekeleka kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo Yanga SC walinufaika na mabadiliko hayo mnamo dakika ya 64 Stephane Aziz Ki alianza kuitanguliza Yanga Sc mbele baada ya kufunga bao zuri akipokea pasi kutoka kwa Tusila Kisinda

Akitokea benchi kiungo Mtukutu Benard Morrison alipigilia msumari wa pili katika dakika za jioni kabisa 90+2′ .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here