
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewateua wafuatao:
i. Amemteua Bw. Tito Philemon Mganwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe; na
ii. Amemteua Bw. Mussa R. Kilakala kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora.
2. Aidha, Mhe. Rais amefanya mabadiliko madogo ya vituo vya kazi kama ifuatavyo:-i.Bw. Athumani Francis Msabila kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga;
ii. Bi. Mwantum Hamis Mgonja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji; na
iii. Bi. Mwamvua Bakari Mnyongo kutoka Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora kwenda kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
No comments:
Post a Comment