SERIKALI YAOMBWA KUTOFAUTISHA KAZI ZA CSO's NA NGO's - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Monday, 23 October 2023

SERIKALI YAOMBWA KUTOFAUTISHA KAZI ZA CSO's NA NGO's

Serikali imeombwa kutofautisha kazi zinazofanywa na Asasi za Kiraia (CSO's), na Asasi zisizo za kiserikali (NGO's) ili kila Mhimili uweze kufanya shuguli zake kwa ufanisi.

Ombi hilo limetolewa na Rais wa foundation for civil society (FCS) Dkt. Stigmata Tenga alipokuwa akifunga rasmi Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI), iliyofanyika kwa juma moja kuanzia Octoba 23 hadi 27, 2023 Katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha.
Amesema kuwa Asasi za Kiraia zitaendelea kuboresha mahusiano mazuri yalipipo kati yao na Asasi zisizo za Kiserikali kwa kuwa wadau wote hao wana jukumu la kuhakikisha wanafanya kazi zao kwaajili ya kuimarisha maendeleo ya Jamii na Taifa kwa ujumla.

"Asasi za Kiraia tutaboresha mahusiano yetu na Asasi zisizo za Kiserikali kwani nchi hii ni yetu, tunaifahamu, na sauti tunazoleta Serikalini ni sauti za wananchi wa nchi hii" amesema Dkt. Tenga.

Ameiomba Serikali kuendeleza ushirikiano na kuwasaidia, kwani wana ajenda nyingi ambazo wanashindwa kuzifanyia kazi kutokana na ushindani uliopo baina ya Asasi hizo.
Katika hatua nyingine, Dkt. Tenga ametangaza kusogezwa muda wa kufanyika Wiki ya AZAKI Kutoka mwezi Octoba kama ilivyo sasa, ambapo kwa mwaka wa 2024, Wiki hiyo itafanyika tarehe 26 hadi 30 mwezi Agosti.

"Tumefanya tathimini ya faida ambayo wana AZAKI wanaipata kwa kushiriki katika makongamano mbalimbali kwa mwaka, na umuhumu wa hayo matamasha yote kupitia kamati tendaji, tunatoa mapendekezo ya kufanya Wiki ya Asasi za Kiraia mwakani, iwe tarehe 26 hadi 30, mwezi Agosti" amesema Dkt. Tenga.

Wiki ya AZAKI 2023 iliyoanza Octoba 23 imehitimishwa rasmi leo Octoba 27, 2023 Jijini Arusha, ambayo imewaleta pamoja Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka Tanzania nzima kwa lengo la kujadili na kuboresha ushirikiano wa kimkakati.
Kauli mbiu ya Wiki ya AZAKI 2023, ni 'Teknologia na Jamii, Tulipotoka, tuilipo sasa na tunapoelekea, kuangazia fursa na changamoto zinazotokana na ulimwengu wa teknolojia unaoendelea'

No comments:

Post a Comment