TADB Yakabidhi Vifaa Na Zana Za Kilimo Kwa Vijana Wa BBT - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 23 January 2024

TADB Yakabidhi Vifaa Na Zana Za Kilimo Kwa Vijana Wa BBT

 Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendajii Frank Nyabundege wamekabidhi vifaa na zana za kilimo kwa vijana 268 wa Programu ya Kilimo Biashara ‘Build a Better Tommorrow – BBT) katika ghafla ya mapokezi na ugawaji vifaa kwa vijana hao iliyofanyika kwenye shamba la Chinangali, Dodoma.


Akizungumza aliyekuwa mgeni rasmi wa ghafla hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Prof. Joyce Ndalichako (Mb), amewataka vijana hao kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kuwahakikishia kuwa BBT ni programu ya kipaumbele.

“BBT ni kati ya vipaumbele vya SerIkali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na niwahakikishie kama Waziri mwenye dhamana ya ajira na vijana serekali itaendelea kuwawezesha vijana kwenye programu hii endelevu,” amesema Mhe.Prof Joyce Ndalichako (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb), alitumia ghafla hiyo kukumbusha na kusisitiza umuhimu na malengo ya kuanzishwa kwa programu ya BBT, amesema kwamba pamoja na kuchochea mageuzi katika kilimo programu pia imelenga kutengeneza ajira, kupunguza umasikini na kuongeza tija kwenye kilimo.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Frank Nyabundege amesema Benki hiyo inatambua na kuthamini jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hasaan katika kuendeleza kilimo nchini kupitia Wizara ya kilimo.

Vilevile aliwahimiza aliwahimiza vijana washiriki wa programu ya BBT kutumia fursa waliyoipata kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikwamua kiuchumi na kutoa wito kwa vijana, wanawake na watanzania kwa ujumla kuchangamkia mikopo inayotolewa na Benki kwenye sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji kwa masharti nafuu.

Nyabundege alihitimisha kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha TADB kutimiza majukumu yake.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege akikabidhi vifaa vya kilimo kwa vijana walio kwenye mpango wa ‘Build a Better Tommorow’iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo katika halfa iliyofanyika jana Chinangali Dodoma. TADB inafadhili vifaa na zana za kilimo zinazotumika kwenye programu hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako (wan ne kushoto), Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wa (kwanza kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege (wa tatu kulia) wakikabidhi vifaa vya kilimo kwa vijana walio kwenye mpango wa ‘Build a Better Tommorow’iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo katika halfa iliyofanyika jana Chinangali Dodoma. TADB inafadhili vifaa na zana za kilimo zinazotumika kwenye programu hiyo.


No comments:

Post a Comment