Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Mpango akishiriki Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Four Points by Sheraton Jijini Dar es salaam tarehe 20 Februari 2024. Kushoto ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Joackim Chissano na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Mpango akipokea Tuzo ya Amani Duniani iliyotolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Four Points by Sheraton Jijini Dar es salaam tarehe 20 Februari 2024. Tuzo hiyo imetolewa na Chuo kikuu cha Dar es salaam kupitia Kigoda cha Uprofesa cha Mwl. Julius Nyerere katika Kiswahili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Mpango akizungumza na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wakuu wa Nchi na Serikali Wastaafu katika Afrika Mhe. Joachim Chissano wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Four Points by Sheraton Jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Mpango akiwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Joackim Chissano, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolph Mkenda, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal cha Afrika Kusini Prof. Nhlanha Mkhize katika picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Four Points by Sheraton Jijini Dar es salaam tarehe 20 Februari 2024.
No comments:
Post a Comment