Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Mkolani Aporinary Mgunda (katikati) akiwa na baadhi ya wanachama wa Tawi hilo kwenye Gereza Kuu la Butimba
Baadhi ya wanachama wa Tawi la Yanga Mkolani wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhi vitu mbalimbali walivyowapelekea wafungwa
Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Mkolani Aporinary Mgunda,Mratibu wa Timu ya Yanga Mkoa Kija Malingwi wakikabidhi baadhi ya vitu ikiwemo mipira ya miguu kwa Mkuu wa Gereza Msaidizi Moshi Mkerya
……………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kuelekea siku ya wananchi (YANGA DAY) itakayofanyika Agosti 4, 2024 Jijini Dar es salaam wanachama wa Tawi la Yanga Mkolani wametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira katika Gereza Kuu la Butimba lililoko Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza.
Vifaa hivyo vimetolewa leo Jumatano Julai 31, 2024
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mratibu wa Timu ya Yanga Mkoani hapa Kija Malingwi, amesema ni utaratibu wao kila inapofika wiki ya wananchi kutembelea vituo mbalimbali kwaajili ya kutoa msaada.
“Leo tumetoa msaada wa vifaa vya michezo hapa Gereza la Butimba vikiwemo mpira, jezi, filimbi, bendera za waamuzi, sabuni pamoja taulo za kike, nitoe wito kwa watu wote wanaoguswa na hawa wafungwa waendelee kutoa msaada ili ndugu zetu waweze kupata mahitaji”, amesema Malingwi
Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Mkolani Aporinary Mgunda, amesema wamekabidhi vifaa vyenye thamani ya laki tisa vitakavyo wasaidia wafungwa hususani katika michezo na mazoezi kwaujumla.
Aidha, ametoa shukrani kwa uongozi wa Magereza kwanamna walivyowapokea vizuri.
Kwaupande wake Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Moshi Mkerya, amefarijika kupokea msaada walioutoa wana Yanga huku akiongeza kuwa wafungwa watacheza na watafanya mazoezi ya viungo.
“Nawashukuru sana wananchi kwa msaada huu wafungwa hawa wanapokuwa Gerezani haimaanishi kuwa hawatakiwi kupata mahitaji muhimu, bali wanatakiwa kupata mahitaji muhimu ikiwemo chakula, michezo ili afya zao zizidi kuimarika, ombi langu kwa jamii waendeelee kutuletee misaada ya vitu mbalimbali vitakavyowasaidia wafungwa”, amesema Mkerya
No comments:
Post a Comment