Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imesaini mkataba wa makubaliano (MOU) na Wakala wa serikali wa uwezeshaji wananchi kiuchumi zanzibar ( ZEEA) Makubaliano haya ya kimkakati yanalenga kuanzisha mpango maalum wa mikopo utakaonufaisha makundi maalum wakiwemo wanawake na vijana wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi visiwani Zanzibar. Mpango huu unakusudia kuchochea ukuaji wa biashara, ongezeko la ajira, na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Akishuhudia kusainiwa kwa hati hizo jijini Dar es salaam Katibu mkuu ofisi ya Raisi kazi uchumi na Uwekezaji zanzibar Mariam amesema tayari shilingi bilioni 2 zimeshakusanywa na halmashauri visiwani humo ili kuanza uwezeshaji akiitaka benki ya TCB kuhakikisha inafanya tathmini ya mikopo wanayotoa kwa makundi hayo ili ziweze kurejeshwa kwa wakati na wengine waweze kukopa .
Ameeleza kuwa mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali,kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao. Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha uchumi wa ndani, kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupambana na ukosefu wa ajira na kuleta maendeleo na kuwa Kupata fursa ya mikopo ni muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa biashara ndogondogo na za kati
Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa TCB ADAM MIHAYO amesema Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla na kwamba Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.
Mpango huu pia utazisaidia biashara kujiendesha, kukabiliana na mfumuko wa bei, pamoja na kuwekeza katika vitendea kazi, na kuzipa ustahimilivu,Tuna furaha kushirikiana na ZEEA kuwainua wajasiriamali wanawake, vijana na makundi mengine maalum yaliyomo visiwani Zanzibar,” alisema Adam Mihayo,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB.
Mchango wa Benki ya TCB katika kuunga mkono jitihada za Serikali katik na kupokea maombi ya mkopo yanayofikia wastani wa Mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali, kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha biashara na uchumi.
No comments:
Post a Comment