Mkuu
wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt.
Henry Mambo akitoa taarifa ya chuo hicho wakati wa uzinduzi wa bodi ya
ushauri ya chuo hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah
Kairuki na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah
Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya
chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi
wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Mkuu wa Chuo na
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Henry Mambo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah
Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya
chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania pamoja na menejimenti ya chuo hicho
wakati wa uzinduzi wa bodi ya chuo hicho mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah
Kairuki (kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Charles Msonde wakati
wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Charles
Msonde (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (kushoto) mara
baada ya uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam,
katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah
Kairuki (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya
Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania mara baada ya kuizindua
mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
Bodi
ya ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) imetakiwa kuhakikisha
inaimarisha utoaji wa elimu bora na yenye viwango kwa watumishi wa umma
ili kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotaka watumishi
wenye weledi na wenye maadili katika sekta za umma na binafsi.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki alipokuwa akizindua Bodi ya
washauri wa chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
Kairuki ameeleza kuwa ni wakati sasa kwa chuo hicho kuwa mfano bora wa
kutoa watumishi ambao watarejesha nidhamu, utumishi bora na uadilifu wa
hali ya juu katika sekta za umma na binafsi ili kumaliza tatizo la
watumishi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo viovu
kama rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.
“Chuo
cha utumishi wa umma hapa nchini kilianzishwa kwa lengo la kutoa mafunzo
kwa watumishi wa umma, hivyo Bodi ya ushauri wa chuo cha utumishi wa
umma wa Tanzania inalo jukumu la kuhakikisha kuwa lengo hili
linatekelezwa kwa ufanisi mkubwa,” alisema Waziri Kairuki.
Aliongeza
kuwa bodi hiyo pia inalo jukumu la kutoa ushauri katika mipango yote ya
maendeleo, kushauri na kupitisha mpango kazi na bajeti ya chuo pamoja
na kufanya tathimini ya mwaka ya utendaji wa chuo na masuala mengine ya
muhimu yanayopaswa kutolewa ushauri.
“Nina
matarajio makubwa kwamba, mtatekeleza majukumu hayo na mengine ambayo
sikuyataja lakini yameelezwa katika sheria husika ili kuhakikisha
kwamba, chuo cha utumishi wa umma kinakidhi matarajio ya serikali pamoja
na wadau na kuleta tija na ufanisi katika utumishi wa umma hapa
nchini,” alifafanua Waziri Kairuki.
Katika
hafla hiyo iliyojumuisha wajumbe waliomaliza muda wao pamoja na wale
waloteuliwa Waziri kairuki alisema kuwa, chuo hakina budi kupunguza kozi
zisizo na soko kwa ajili ya kutoa elimu kwa ufanisi na tija kwa
wanafunzi kama ilivyo kusudi la kuanzishwa kwa chuo hicho ambalo ni
kutoa elimu kwa watumishi wa umma.
Aidha
Waziri Kairuki amewapa changamoto wajumbe wa bodi hiyo walioteuliwa
katika bodi hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia, uendelevu wa chuo
(Sustainabilty), kujitangaza kwa chuo ili kuongeza idadi ya wanafunzi,
kozi gani zinazoweza kuwavutia wanafunzi, kufanya tathmini ya wanafunzi
wanaohitimu chuoni hapo kama wanakidhi vigezo katika ofisi za waajiri wa
ofisi za umma na zile za binafsi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Dkt. Henry Mambo
alisema kuwa kwa sasa chuo hicho kimefanikiwa kutoa mafunzo ya muda
mfupi kwa watumishi, kutoa machapisho mbalimbali ya ndani na nje,
kuanzisha kozi za shahada na kuongeza idadi ya wahitimu.
Dkt.
Mambo alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho kimeweza kutoa
mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi takribani 58221, katika Nyanja za
uongozi, menejimenti na utawala bora, chuo kinadahili na kutoa mafunzo
ya muda mrefu kwa watumishi wa umma na watumishi tarajali wapatao 132890
na kati ya hao watumishi wa umma wanatarajia kuwa 29240 ambayo ni sawa
na asilimia 22.
Naye
Mwenyekiti mteule wa Bodi hiyo Dkt. Charles Msonde alisema kuwa
atashirikiana na wajumbe, watendaji na Wizara ya utumshi kuendeleza
mafunzo bora kwa watumishi wa umma ili kuendana mabadiliko ya sayansi na
teknoljia pamoja na uhitaji wa soko hapa nchini na nje ya nchi.
Bodi
hiyo inaundwa na wajumbe sita ambao ni Dkt. Charlse Msonde (Mwenyekiti),
na Prof. Bernadetha Killian,Bibi. Anna Maembe, John Ullanga, Solanus
Nyimbi, Bi. Roxana Kijazi
Chuo
cha utumishi wa Umma kilianzishwa mwaka 2000 kwa lengo la kutoa elimu na
mafunzo kwa watumishi wa umma hapa nchini na nje ya nchi,chuo hiki kipo
chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, kina matawi sita katika mikoa ya Mbeya, Dar es Salaam (Magogoni),
Mtwara, Singida, Tabora na Tanga

No comments:
Post a Comment