Dkt. Kigwangalla - Tanzania na Oman kushirikiana kwenye Utalii wa Kihistoria na Utamaduni - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Thursday, 19 October 2017

Dkt. Kigwangalla - Tanzania na Oman kushirikiana kwenye Utalii wa Kihistoria na Utamaduni

  1. aziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema  Tanzania na Nchi ya Oman zimefanya mazungumzo katika kuimalisha sekta ya Utalii hasa kwenye Utalii wa kukuza Utamaduni na ule wa Kihistoria uliokuwepo miaka mingi kwa Mataifa hayo.
  2. Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla amebainisha hayo jioni ya jana Oktoba 18,2017, wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho ya nyimbo na ngoma za Taifa la Oman yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam ambapo pia tukio lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na viongozi wa Taifa hilo la Oman ambao wapo Nchini kwa ziara ya kusambaza Ujumbe wa Amani na Upendo kupitia meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’.
  3. Akizungumza mara baada ya kushuhudia maonyesho ya ngoma na nyimbo hizo za Taifa la Oman, Dkt. Kigwangalla amebainisha kuwa, Watanzania wameweza kujifunza na kufurahia utamaduni wa Oman hasa kupitia nyimbo, ngoma na mashahiri ambapo amebainisha kuwa Serikali itaendeleza ushirikiano mwema hususani wa Kiutaduni na kukuza Utamaduni.
  4. “Watanzania na watu wa Taifa la Oman ni ndugu. Hivyo kupitia ngoma  na nyimbo hizi walizoonesha hapa zinafanana sana za zile za Visiwa vya Zanzibar na ukanda wetu huu wa Pwani wa Tanzania.
  5. Pia hata baadhi ya viongozi waliokuja na msafara huu wanazungumza vizuri lugha ya Kiswahili bila kuchanganya na lugha nyingine huku wengine kama mulivyowaona wana asili ya Tanzania ikiwemo Visiwa hivyo vya Zanzibar ambapo walizaliwa huko.” Ameeleza Dkt. Kigwangalla.
  6. Aidha, ameeleza kuwa, kwa sasa wanakusudia kutengeneza chanzo kipya cha Utalii ambacho kitakuwa ni cha Kihistoria na Kiutamaduni baina ya Mataifa hayo mawili  na kufafanua kuwa, Histoia ya Tanzania hasa Lugha ya Kiswahili huwezi kukitenganisha Bara la Arab hususani watu wa Oman.
  7. “Kuna wengine wasomi wa Historia na utamaduni wa Uislamu wamebainisha kwenye taarifa za kisayansi, kuwa pengine hata dini ya kiisilamu ilianza kufika ukanda wa Pwani wa Afrika Mashariki kabla ya hata haijafika baadhi ya Nchi ya Mashariki ya Kati.
  8. Hii ni pamoja na makaburi ya kale kule Bagamoyo, Pemba na sehemu nyingine za Tanzania ambapo kwa pamoja yanaonesha uwepo wa Waislamu na mashekhe wa kiisilamu waliofika kuanzia mwaka 1200 mpaka hadi 2000, miaka mingi iliyopita.” Alibainisha Dkt. Kigwangalla.
  9. Ameongeza kuwa: “Wao wakitangaza vivutio vyao, watavitangaza na vivutio vyetu vya Tanzania. Lakini pia sisi tutatumia fursa vivutio tulivyonavyo ambavyo wao hawana kama Mbuga za Wanyama kuwaalika watu wa Omani kuja kutalii Tanzania, kipindi cha Mwezi Juni, Julai hata Agosti wao ni kipindi cha joto kali kwani wakati mwingine  msimu huo kule wao wanakuwa na utaratibu wa kutoa rikizo ama mapumziko ya muda wa zaidi ya siku 30 hadi 40 hivyo tutatumia  fursa ya kipindi hicho na hata wale wanaowapokea Oman waweze kuja Tanzania kutalii” alieleza.
  10. Pia alimalizia kwamba,  ushirikiano huo, utaongeza soko kubwa la kiutalii.
  11. Msafara huo wa viongozi wa Oman wakiwemo Mawaziri na wafanyakazi wa Meli hiyo ya Mfalme wa Taifa hilo unajumuisha watu zaidi ya 300 ambapo leo Oktoba 19,2017, umetembelea Wilaya ya Bagamoyo kujinea fursa za kiuwekezaji na uchumi katika ukanda huo wa Pwani huku Meli hiyo kesho Oktoba 20,2017 ikitarajiwa kuondoka kuelekea Mombasa Nchini Kenya.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, Kulia ni Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman Dkt. Mohamed Hamad Al Rumhy alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, alipokuwa akiwasili kwenye tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akiteta jambo pamoja na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, wakati akishuhudia tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akiongea  na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily, wakati akishuhudia tukio la Ngoma na nyimbo za Taifa la Oman, Jijini Dar es salaam
 Bendi ya Jeshi la Taifa la Oman wakipiga nyimbo za Taifa hilo zinazofanyika wakati wa vita na ukombozi
 Baadhi ya wananchi wakiwa na bendera za Taifa la Oman na Tanzania wakishuhudia tukio hilo
 Baadhi ya Askari wa kikosi Maji cha Oman wakiwa katika tukio hilo.
 Dkt. Kigwangalla akizungumza na wanahabari 
 Dkt. Kigwangalla akizungumza na wanahabari 
 Dkt. Kigwangalla akizungumza na wanahabari 
 Kikundi cha utamaduni  cha Oman wakionesha ngoma za Utamaduni wa Taifa hilo.
 Kikundi cha utamaduni  cha Oman wakionesha ngoma za Utamaduni wa Taifa hilo.
 Kikundi cha utamaduni  cha Oman wakionesha ngoma za Utamaduni wa Taifa hilo.
Kikundi cha utamaduni  cha Oman wakionesha ngoma za Utamaduni wa Taifa hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here