Mawakala
wa benki ya CRDB kupitia huduma ya Fahari Huduma kutoka wilaya zote za
mkoa wa Mwanza, wakiwa kwenye semina iliyoyandaliwa na benki hiyo kwa
ajili ya kuwajengea weledi na uwezo wa kutoa huduma bora kwa wateja.
Mawakala
kutoka wila ya za Nyamagana, Ilemela, Magu, Misungwi, Kwimba, Sengerema
pamoja na Ukerewe walihudhuria kwenye semina hiyo iliyofanyika alhamisi
iliyopita Oktoba 12,2017 Jijini Mwanza.
Akifungua
semina hiyo, Mkurugenzi wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Wambura
Calystus aliwasihi mawakala hao kuwa waaminifu katika kuwahudumia wateja
ikiwemo kutunza siri za mihamara ya pesa za wateja wao huku wakitoa
huduma bora kama ilivyo ada ya benki ya CRDB wanayoiwakilisha katika
maeneo yao.
Mawakala
hao walieleza kwamba semina hiyo itawasaidia kuboresha huduma zao kwa
wateja na hivyo kuwahimiza wateja wa benki ya CRDB kuendelea kutumia
huduma za benki hiyo kwani zinapatikana kwa urahisi katika maeneo yote
nchini.
Mkurugenzi wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Wambura Calystus, akifungua semina hiyo
Meneja wa CRDB tawi la Nyanza Jijini Mwanza, Mafwimbo Mulungu akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa wa CRDB, Danford Muyango akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa BIMA kutoka benki ya CRDB tawi la Nyanza, Jackline Jubilate akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo
Mmoja wa maofisa wa benki ya CRDB, akizungumza kwenye semina hiyo
Meneja biashara wa CRDB tawi la Nyanda, Eugenius Mashishanga (kushoto), akizungumza kwenye semina hiyo
Baadhi ya wakala wa CRDB wakichangia mada kwenye semina hiyo
Baadhi ya mawakala wa benki ya CRDB wakiwa kwenye semina hiyo
Bonyeza HAPA CRDB ilivyoadhimisha Wiku ya Huduma kwa Wateja Geita
No comments:
Post a Comment