Hafla ya uapisho huo ilifanyika Ikulu, Zanzibar kwa kuratibiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmeid Said.
Walioapishwa ni Dk. Habiba Hassan Omar, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ambae amechukua nafasi ya aliekua katibu wa Wizara hiyo, Dk. Mngereza Mzee Miraji alieteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya. Awali Dk. Habiba alikua Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
Rais Dk. Mwinyi pia amemuapisha Dk. Mngereza Mzee Miraji kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, kabla ya nafasi hiyo, Dk. Miraji alikua Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.
Pia Dk. Mwinyi amemuapisha ndugu Maryam Juma Abdalla Saadalla kuwa Katibu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, kabla ya nafasi hiyo Maryam alikua Katibu Mkuu (Kazi na Uwezeshaji) katika Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemuapisha Khamis Suleiman Mwalim kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji. Kabla ya nafasi hiyo, Khamis alikua Katibu Mkuu (Uchumi na Uwekezaji) katika Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji.
Hafla ya uapisho huo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Sulemain Abdulla, viongozi wa dini pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment