AMPUNI ya Huawei, yenye makao yake makuu mjini Shenzhen nchini China, inatarajia kuutambulisha mpango wake wa utoaji elimu kwa njia ya Tehama, unaojulikana kwa jina la E-education.
Hayo
yalibainishwa mapema wiki hii na maofisa kutoka kampuni hiyo wakati wa
ziara ya waandishi wa habari nchini China waliotembelea kujionea namna
mradi ‘Smart education’ wanaoutekeleza katika shule ya msingi Baogang
nchini China na kuwa wa mafanikio.
Meneja
Mahusiano wa kampuni hiyo, Schloss glenn James, alisema kuwa kuanzishwa
kwa mradi kama huo wa elimu kwa njia ya teknolojia ya Tehama kwa shule
za msingi na sekondari itasaidia kuinua kiwango cha elimu nchini kama
ilivyothibitika katika mradi ulioanzishwa katika shule ya msingi
Baogang.
James
alisema Huawei kwa sasa wamejikita zaidi katika miradi ya mifumo ya
elimu kwa mtandao ambapo kupitia mradi huu, matarajio ni kuboresha
kiwango cha elimu kwa kiwango cha juu kupitia teknolojia ya Tehama kwa
ajili ya kufundishia na kusoma.
Kwa
mazingira hayo, Huawei wamekuwa wakihamisha ujuzi wao kwenda kwa
watumishi mbalimbali nchini kwa kuwatumia wataalamu waliobebea ndani ya
Huawei.
Meneja
huyo alisema katika kutekeleza jukumu hilo, Huawei ikiwa na watumishi
120, wamekuwa wakitoa mafunzo na elimu kwa vitendo kwa wanafuzni wa fani
ya Tehama.
Sambamba
na hayo, mkakati wa kampuni hiyo ya Huawei, ni kupanua wigo wao katika
uboreshaji wa miundombinu ya ICT kwa lengo la kuiunganisha nchi ya
Tanzania.
Alifafanua
kwamba ajenda ya kampuni hiyo ni kuhakikisha wanaendelea kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi wa kiwango cha kimataifa katika kuyafikia
mageuzi ya kweli katika nyanja mbalimbali kupitia utaalamu wa teknolojia
ya tehama.
Kwa
mwaka huu, Huawei wamekuwa katika mkakati kamambe wa kutafuta njia
mbadala na bora zaidi za kuisaidia Serikali katika malengo yake yake ya
kiuchumi ifikapo mwaka 2020/2025.
Huawei
wamekuwa wakifanya hivyo kwa maslahi ya nchi katika kutimiza wajibu wao
wa kuhakikisha vyanzo na njia mpya za kuharakisha maendeleo
zinapatikana.
No comments:
Post a Comment