Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa
wake wa Twitter na kusema tabasamu la Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu akiwa kwenye hospitali jijini Nairobi linatoa matumaini
makubwa.
"Mjomba tunamshukuru Mungu kwa tabasamu
hili la matumaini!Nakuombea afya iimarike kabla hujasema mengi! Tulia
mjomba upone kabisa kwanza" alisema Nape Nnauye
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
alishambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma
nyumbani kwake na baadaye alipelekwa jijini Nairobi kwa matibabu zaidi
ambapo mpka sasa anapatiwa matibabu huko.
No comments:
Post a Comment