Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 72 ya umoja wa Mataifa UN
yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 24 mwaka huu katika ukumbi wa Kareemjee
jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini humo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Susan Kolimba amesema kuwa zaidi ya
watu 500 wanatarajiwa kushiriki katika maadhimisho hayo wakiwemo
watumishi wa Serikali,mabalozi wa nchi mbalimbali,wanafunzi,vyombo vya
Usalama ,wadau mbalimbali pamoja na wananchi walioalikwa kuhudhuria
katika siku hiyo.
Pia
amesema kuwa UN kwa kupitia Taasisi zake wameweza kutoa misaada
mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na kutoa dollar za kimarekani
laki 1 sawa na Milioni 220 za kitanzania katika chuo cha Polisi Moshi
ili kuwajengea uwezo walimu kuweza kupambana na ukatili kwa wanawake na
Watoto.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa UN nchini ALVARO RODRIGUEZ amesema kuwa
wataendelea kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ya Tanzania pamoja na
wadau wa maendeleo ili kuweza kuleta maendeleo hapa nchini.
Mbali
na maadhimisho hayo kufanyika jijini Dar es salaam lakini pia
yatafanyika Zanzibar Oktoba 26 mwaka huu katika hotel ya Serena na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa.
No comments:
Post a Comment