Hatua
hiyo ni utekelezaji wa sheria mpya za madini ya Tanzania baada ya
kampuni hiyo kukubali kuwa na mazungumzo na Serikali ya Tanzania .
Vilevile
kampuni hiyo imekubali kutoa Dola za Kimarekani milioni 300 kama malipo
ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa
mapato kutokana na biashara ya kampuni hiyo.
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni hiyo,Prof. Thornton amesema Barrick Gold
Corporation watazingatia makubaliano haya na wanaamini kuwa yamefungua
ukurasa muhimu utakaowezesha kufanya biashara kisasa.
Kwa
upande wake Rais wa Tanzania John Magufuli amesema makubaliano hayo
yataisaidia nchi kuzalishaji ajira zaidi, kupata manufaa mbalimbali
yanayostahili ikiwemo fedha za kugharamia huduma za kijamii kwa wananchi
na yanajenga msingi imara ambao utaiwezesha Tanzania kunufaika na
rasilimali zake za madini.
Wakati
huohuo waziri wa Katiba na Sheria nchini humo Prof.Palamagamba Kabudi
ambaye alikuwa kiongozi wa mjadala huo amesema sheria hiyo iliyopita
mwezi july imeleta dira mpya katika biashara hiyo ya madini.
No comments:
Post a Comment