Watano mbaroni kwa mauaji - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 4 October 2017

Watano mbaroni kwa mauaji

Watano mbaroni kwa mauaji
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu watano ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kikatili ya Afisa Tarafa ya Lupiro wila...
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu watano ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kikatili ya Afisa Tarafa ya Lupiro wilayani Ulanga ambaye aliuawawa kwa kupigwa mapanga na shoka na watu wasiojulikana. 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira amethibitisha kukamatwa kwa watu hao watano na kusema sasa wanaendelea kufuatilia watu wengine waliohusika kwenye shambulio hilo na kusema kuwa upelelezi bado unaendelea na pindi utakapokamilika watuhumiwa hao watapelekwa kwenye vyombo vya sheria za hatua nyingine zaidi. 

"Ni kweli tumewakamata watu watano ila kwa sasa hatuwezi kuwataja kwa majina kwa kuwa upepelezi bado unaendelea na pindi utakapokamilika basi tutawafikisha mahakamani kwa hatua nyingine za kisheria" alisema Leonce Rwegasira

Aidha Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira amesema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea na upelelezi juu ya tukio hilo na matukio mengine mbalimbali ambayo yametokea mkoani Morogoro. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here