WATUHUMIWA
watatu kati ya 11 wanao shikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa
Kilimanjaro kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya
Scolastica, Humphrey Makundi, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
,Moshi na kusomewa shtaka la mauaji.
Washitakiwa
wawili Hamis Chacha aliyekuwa mlinzi wa shule ya Skolastica na Labani
Nabiswa walifikishwa mahakamani hapo wakitokea kituo kikuu cha kati cha
Polisi wakiwa chini ya ulinzi mkali.
Baada
ya nusu saa Mmiliki wa shule ya Scolastica ,Edward Shayo alifikishwa
mahakamani hapo na askari Kanzu akitokea Hospitali ya Rufaa ya KCMC
alipokuwa akipatiwa matibabu ya baada ya kupata tatizo la kiafya tangu
kushikiliwa kwake.
Upande
wa Jamhuri katika shtaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi ,Julieti
Mawore umewakilishwa na Mwanasheria Kassim Nassiri akisaidiana na
Wakili wa kujitegemea Faygrace Sadallah huku upande wa utetezi
ukiwakilishwa na Wakili Eliakunda Kipoko anyemtetea Mshatakiwa wa pili
katika shtaka hilo Edward Shayo.
Akisoma
maelezo ya hati ya mashtaka mbele ya mahakama hiyo Nassiri alieleza
kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshtakiwa wa kwanza ,Hamis Chacha(28),wa
pili Edward Shayo (63) na wa tatu Laban Nabiswa (37) walimuua kwa
kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.
Kutokana
na maelezo hayo Hakimu Mawore alieleza kuwa washtakuwa hawaruhusiwi
kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya
kusikliza shtaka la mauaji huku akiwataka kungojea kufanya hivyo pindi
watakapofikishwa mahakama kuu ambapo watapata nafasi ya kuwasilisha
mashahidi wao pamoja na kujitetea.
Kuhusu
upelelezi wa Shtaka hilo Mwanasheria wa serikali Nassiri aliieleza
mahakama kuwa upelelezi haujakamilika huku akiwasilisha ombi la kupangwa
tarehe nyingine kwa ajili kutajwa kwa shauri hilo wakati upelelezi
ukikamilishwa.
Hakimu
Mkazi Mawore aliahairisha shtaka hilo na kupanga kutajwa Desemba 8
mwaka huu na kwamba washtakiwa wote watarudishwa Rumande kutokana na
kesi hiyo kutokuwa na dhamana.
Washatakiwa
hao wamefikishwa mahakamani zikiwa zimepita siku 11 tangu kufukuliwa
kwa mwili wa mtu aliyezikwa na Halmashauri ya Manspaa ya Moshi kuondoa
utata wa kupotea kwa Mwanafunzi Humphrey Makundi (16) aliyekuwa anasoma
shule ya sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo mkoani
Kilimanjaro.
Mahakamani ya Hakimu mkazi, Moshi.
Anayetajwa kuwa mmilikiwa wa shule ya sekondari ya Scolastica Edward Shayo akifikishwa katika mahakamani ya Hakimu mkazi Moshi.
Anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scolastica, Edward Shayo akijiandaa kuingia chumba cha mahakama Jana.
Anayetajwa
kuwa mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo mji ndogo wa
Himo Edward Shayo na wenzake wawili Hamid Chacha na Laban Nabiswa
wakisindikizwa kuingia chumba cha mahakamani.
Anayetajwa
kuwa mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Scolastica Edward Shayo na
wenzake wawili wakitoka nje ya chumba cha mahakamani Mara baada ya
kusomewa shtaka la kuua kwa kukusudia .
Mmoja wa ndugu wa kijana Humphrey Shayo akilia kwa uchungu wakati akitoka katika chumba cha mahakama
Ndugu
wa anayetajwa kuwa mmiliki wa wa shule ya Sekondari ya
Scolastica,Edward Shayo wakionekana kwenye huzuni Mara baada kusomewa
kwa mashtaka ya mauaji kwa ndugu yao h
No comments:
Post a Comment