MWENYEKITI
wa Shirikisho la Waganga wa Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA)
Abdallahaman Lutenga Amesema chini ya uongozi wake atahakikisha hakuna
fisadi wala mchwa yeyote atakaengia kwenye shirikisho hilo.
Amesema
kuwa wanachama wa shirikisho hilo lazima watambue kuwa shirikisho hilo
ni mahala patakatifu na viongozi wanaokwenda kuongoza shirikisho lazima
wawe waadilifu na wenye uchungu na si vinginevyo.
Lutenga
ametoa kauli hii mapema leo katika mahojiano maalum ambapo alikuwa
anajibu hoja mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya wanachama wa
shirikisho hilo.
Amesema
kuwa anasikia malalamiko na hoja ambazo zinatolewa na baadhi ya waganga
hususani wakihoji uhalali wa yeye kuendelea kuwa Mwenyekiti ambapo
amesema yeye yupo kwa mujibu wa Katiba yao na Kama kuna watu hawataki
basi wanaweza kwenda Mahakamani.
Mwenyekiti
huyo taifa amesema kuwa yeye ataendelea kuwa mwenyekiti hadi uchaguzi
Mkuu wa shirikisho hilo utakapofanyika mwishoni mwa 2018 nakudai kuwa
wajumbe wa halmashauri kuu kwa mujibu wa katiba yao kwa Kauli moja
waliwaongezea muda ili kukamilisha baadhi ya mambo.
"Nataka
nikuambie ndugu mwandishi unajuwa kuna watu wachache wanaleta vurugu
ili uonekane kuna mgogoro ndani ya shirikisho lakini kikubwa watu
hawasomi katiba inaelekeza nini. "amesema Lutenga
Nakuongeza
kuwa kama kuna watu wanataka uongozi wasubili hadi muda
utakapofikat.nakwamba hata hivyo muda ukifika chini ya uongozi wake
hakuna majizi wala mafisadi watakaopewa nafasi ya kuingia kwenye
uchaguzi huo.
Lutenga
amesema anawasikia baadhi ya wanachama kuhoji kwanini yeye anakwenda
mikoani kufanya kazi za shirikisho lakini wanasahau kama mimi ndio
msemaji wa shirikisho hilo na ndio anateua viongozi wa mikoa na Wilaya
kwa mujibu wa katiba yao
"Sikiliza
nikuambia Mwandishi hawa watu wanamatatizo na tatizo kubwa hawasomi
katiba yetu hivyo ninachofanya kupo ndani ya katiba. Narudia tena hakuna
dili wala rushwa hapa. na wote ambao wanakwenda kinyume na taratibu
zetu sitawaonea haya. "amasema Lutenga.
Lutenga
ametoa rai kwa wanachama wake kuendelea kuheshimu katiba na kama kuna
watu wanadhan yeye anavunja katiba basi wasikae kupiga majungu bali
waende Mahakama lakini si kupiga kelele kwenye miitandao na vyombo vya
habari.
No comments:
Post a Comment