MKOA wa Mwanza umefanya Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji ambao umeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF). Mwongozo
huo ni sehemu ya ripoti tatu zilizotokana na agizo la mkoa wa Mwanza la
kutaka kuwekewa pamoja taarifa sahihi zinazogusa uwekezaji mkoani humo
ili kurahisisha na kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje. Ripoti
nyingine ni Fursafiche katika Viwanda (Industrialization Potentials
Report), na Ripoti ya Fursa za Uwekezaji (Investment Opportunities
Report) .
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi
wa serikali, Mashirika ya Umma, Sekta binafsi na mashirika ya kimataifa,
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella, alisema walilazimika
kuwatafuta wataalamu wa ESRF, kuwasaidia kuweka pamoja fursa zote za
mkoa katika mpangilio mmoja unaobainisha fursa zilipo. Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitoa hotuba ya uzinduzi wa
Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo uliondaliwa na ESRF kwa chini ya
ufadhili wa UNDP katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi
ya Mkuu wa Mkoa jijini Mwanza.
Alisema
katika kukabiliana na changamoto hizo waliiomba Taasisi hiyo kufanya
utafiti na uchambuzi wa kina ili kubaini fursa za uwekezaji zilizopo
katika Mkoa huo na ndio wakatoka na ripoti tatu ikiwa Mwongozo huo.Alisema
kazi hiyo ilifanyika kwa miezi 4 kwa msaada wa kifedha kutoka Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuanzia mwezi Julai 2017 hadi
Novemba 2017. Mongela alisema:
wawekezaji wamekuwa wakipata taabu namna ya uoanishaji wa taarifa
zinazotolewa kwao kutoka mamlaka moja hadi nyingine. Mkurugenzi
Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akitoa taarifa kuhusu uandaaji wa Mwongozo wa Uwekezaji mkoani
Mwanza ulioandaliwa na taasisi yake katika hafla fupi ya uzinduzi wa
mwongozo huo uliofanyika jijini Mwanza.
Alisisitiza
katika hotuba yake kuwa wawekezaji walikuwa wanapata majibu tofauti
katika maswali yao walipofika katika mkoa huo kutoka kwa watendaji
tofauti ambao ilikuwa lazima kuwaona ili kukamilisha nia yao ya kuwekeza
. Alisema kutokana na hali hiyo
waliomba ESRF kuwasaidia kuweka pamoja takwimu zote na kuwavutia
wawekezaji kwa kuwa na majibu ya maswali muhimu wanayotakiwa kuyajua
kabla ya kuwekeza.Mongela alisema
kwamba mwongozo uliotengenezwa unakwenda sanjari na dira ya maendeleo ya
Tanzania na kuwataka wawekezaji wa kigeni na nchini kuwekeza katika
mkoa huo. Mkuu
na Mtaalamu wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) Tanzania, Bw. Amon Manyama akitoa salamu za UNDP katika hafla
fupi ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza uliofanyika
kwenye viwanja vya ofisi za Mkuu wa Mkoa huo jijini Mwanza.
Alisema
wakiwa katikati ya nchi za Afrika Mashariki, zenye soko la watu wapatao
milioni 230, Mwanza ni sehemu muhimu na njema kabisa kwa uwekezaji. Akitoa
taarifa ya utekelezaji wa kazi waliyopewa Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi
Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) alisema pamoja
na kukabidhi mwongozo huo, Ripoti zote zilithibitishwa na Mkoa Septemba
15, 2017 katika warsha maalum iliyoandaliwa na Mkoa (Validation
Workshop).
Tayari ESRF imeshandaa na kuzindua Mwongozo kama huo Mkoani Simiyu mwanzoni mwa mwaka huu. ESRF
imeshakamilisha kuandaa Miongozo ya Uwekezaji katika Mikoa ya Mara na
Kilimanjaro ambayo inatarajiwa kuzinduliwa ndani ya wiki mbili zijazo.
Miongozo hii itasaidia sana katika kupata Mwongozo wa Uwekezaji wa Taifa
utakaoonyesha fursa zilizopo nchini na katika kila mkoa.” Alisema Dkt
Kida. Mshiriki
Mtafaifiti wa ESRF, Dkt Hoseana Lunogelo, akiwasilisha fursa za
uwekezaji mkoani Mwanza walizoziona wakati wa kuandaa Mwongozo wa
Uwekezaji wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mwongozo huo
jijini Mwanza.
Miongozo
hiyo ya Uwekezaji, alisema Dkt. Kida inaendana na Dira ya Maendeleo ya
Taifa 2025 na Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016
– 2021) unaosisitiza ujenzi wa Tanzania ya Viwanda ili kuifikisha nchi
katika uchumi wa kati ifikapo 2025. Pamoja
na kutoa maelezo ya kazi Dk Kida alishukuru uongozi wa mkoa wa Mwanza
na taasisi zake mbalimbali kwa kuwezesha ukusanyaji wa takwimu na
kuandaa muongozo huo.
“Kwa
namna ya pekee napenda kuushukuru Uongozi wa Mkoa wa Mwanza chini ya
Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa John Mongella, Katibu Tawala wa Mkoa – Kamishna
wa Jeshi la Polisi Bw. Clodwing Mtweve na viongozi wengine wa mkoa na
wilaya zote kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wataalamu wetu wakati
wanapita kutafuta maoni, taarifa na takwimu mbalimbali za kutayarishia
Mwongozo huu.” Alisema Dkt. Kida na kuwashukuru pia Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa ufadhili wa fedha. Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (wa tatu kulia),
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),
Dkt. Tausi Kida (katikati), Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF
Bi. Margareth Nzuki (wa pili kulia), Mkuu na Mtaalamu wa Miradi kutoka
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Bw. Amon
Manyama (wa tatu kushoto), Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Hoseana
Lunogelo (wa pili kushoto) Watafiti vijana kutoka ESRF Bw. Mussa Martine
(kushoto) pamoja na Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani (kulia) wakiwa
kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wameshika nakala za Mwongozo wa
Uwekezaji wa Mkoa wa Mwaza.
“Napenda
kuishukuru timu yangu ya ESRF ikiongozwa na Bi. Margareth Nzuki, Mkuu
wa Idara ya Maarifa na Ubunifu kwa kuratibu na kuongoza zoezi zima,
watafiti washiriki kuanzia na Dkt. Hoseana Lunogelo, Prof. Haidari Amani
na Prof. Samuel Wangwe kwa kupitia mwongozo huu.”
Alisema na kuwashukuru watafiti vijana waliojitoa kwa nguvu zote kufanikisha kazi hiyo. Aliwataja vijana hao kuwa ni Bw. Mussa Martine, Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani pamoja na Bw. Hafidhi Kabanda . “Aidha, natambua mchango mkubwa aliotoa marehemu Abdallah Hassan katika uandaaji wa Mwongozo huu.” Alisema. Aidha
alisema kazi hiyo ilifanyika kwa kushirikisha wadau kutoka Sekretarieti
ya Mkoa; Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza, yaani Mwanza Mjini, Magu,
Kwimba, Sengerema, Buchosa, Ukerewe, Ilemela na Misungwi; pamoja na
wadau kutoka Sekta binafsi. Mwenyekiti
wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini (CTI), Dkt. Samuel Nyantahe
akitoa neno la shukrani kutoka CTI wakati hafla ya uzinduzi wa Mwongozo
wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza uliofanyika katika viwanja vya ofisi za
Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Aidha
Mkurugenzi huyo aliutaka mkoa kutosita kuwatumia pale wanapohitaji
msaada wa kitaalam katika utekelezaji wa Mwongozo na hata kusaidia
katika kufanya upembuzi yakinifu (Feasibilty Study) na kuandaa Business
Plans kwa baadhi ya fursa ambazo Mkoa utapenda kuwekeza. Naye
Amon Manyama, Mkuu na Mtaalamu wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania akizungumza alipopewa nafasi
aliwahimiza wananchi wa mwanza kutumia fursa zilizopo kuwekeza badala ya
kuwaachia wageni pekee. Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga
akisisitiza jambo kwenye hafla ya uzinduzi wa Mwomgozo wa Uwekezaji wa
mkoa wa Mwanza uliondaliwa na ESRF chini ya ufadhili wa UNDP jijini
Mwanza.
Alisema
kwamba shirika lake litaendelea kushirikiana na Mwanza katika
kuhakikisha kwamba Jiji hilo linaipiku Dar Es Salaam katika uchumi kwa
kusaidia kupata wawekezaji wenye uhakika kutoka hata ughaibuni. Alisema
Mwanza ikiwa katikati ya Afrika Mashariki ina kila nafasi ya kukua kwa
kasi na wao kama UNDP watahakikisha kwamba wanatoa ushauri wa namna ya
kujenga uchumi kwa kutumia sekta binafsi na namna ya kushirikiana na
taasisi za kitafiti kama ESRF. Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa
Ilemela jijini Mwanza, Mh. Angelina Mabula akizungumza kwa niaba ya
Wabunge wa jijini humo mara baada ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji
wa mkoa huo uliofanyika katika viwanja vya ofisi za Mkuu wa mkoa wa
Mwanza. Picha
juu na chini ni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella
(wa tano kulia) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa sita kushoto) kwa pamoja wakizindua
Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Mwanza iliyoandaliwa na ESRF na kufadhiliwa
na UNDP.
Wanaoshuhudia
tukio hilo ni Mkuu na Mtaalamu wa Miradi UNDP Tanzania, Amon Manyama
(wa nne kushoto), Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI)
Dkt. Samuel Nyantahe (wa tano kushoto), Kamishna wa Jeshi la Polisi Bw.
Clodwing Mtweve (wa pili kulia) pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini
na wa mkoa wa Mwanza katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.[caption id="attachment_3222" align="aligncenter" width="1404"] Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella na meza kuu wakionyesha
nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo baada ya kuzinduliwa rasmi
katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza.Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella katika picha ya pamoja
na Wakuu wa wilaya za jiji la Mwanza huku wakiwa wameshika nakala za
Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza uliondaliwa na ESRF chini ya
ufadhili wa UNDP. Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella katika picha ya pamoja
na taasisi za sekta binafsi yakiwemo mabenki na mifuko ya jamii mara
baada ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza. Picha
juu na chini ni Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella
katika picha ya pamoja na wawekezaji wa jijini Mwanza mara baada ya
kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza. Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa
Ilemela jijini Mwanza, Mh. Angelina Mabula (wa kwanza kushoto) akifurahi
jambo wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza
uliondaliwa na ESRF na kufadhiliwa na UNDP. Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (wa tatu kushoto),
Kamishna wa Jeshi la Polisi Bw. Clodwing Mtweve (wa pili kushoto),
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),
Dkt. Tausi Kida (wa tatu kulia), Mkuu na Mtaalamu wa Miradi kutoka
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Bw. Amon
Manyama (wa pili kulia), Kiongozi wa dhehebu ya dini Kiislamu pamoja na
Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini (CTI), Dkt. Samuel
Nyantahe wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mwanza.[/caption] [caption id="attachment_3237" align="aligncenter" width="1404"]Mshiriki
Mtafaifiti wa ESRF, Dkt Hoseana Lunogelo (wa kwanza kushoto), Mkuu wa
Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Margareth Nzuki (katikati) na
Mtafiti Mshiriki Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani wakifuatilia shughuli
mbalimbali zilizokuwa zikijiri kwenye uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji
wa Mkoa wa Mwanza ulioandaliwa na ESRF na kufadhiliwa na UNDP.Wakuu wa Wilaya za Mikoa ya Mwanza walioshiriki uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza.[/caption] [caption id="attachment_3231" align="aligncenter" width="1404"]Pichani
jiuu na chini ni baadhi ya wadau kutoka sekta binafsi na serikali
waliohudhuria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza
uliondaliwa na ESRF na kufadhiliwa na UNDP ambapo uzinduzi huo
umefanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.[/caption]
No comments:
Post a Comment