Uchaguzi ulifanyika katika kata 43 zilizo kwenye halmashauri 36 za mikoa 19 nchini.
Akizungumza leo Alhamisi Novemba 30,2017
Kaimu Mtendaji Mkuu wa LHRC, Anna Henga amesema uchaguzi ulikuwa na
matumizi mabaya ya vyombo vya dola, watu kupigwa, kukamatwa na
kujeruhiwa.
"Vitendo hivi vimeripotiwa kufanywa na
vyombo vya dola, watu wasiojulikana na watu wanaosadikiwa kuwa ni
wafuasi wa vyama vya siasa vikiwemo CCM na Chadema,” amesema.
Amesema kutokana na matukio hayo, vyombo
vya dola vinapaswa kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua kali za
kisheria kwa watakaobainika kuhusika kwa njia moja au nyingine.
Henga amesema matukio hayo yasipokemewa
ni kiashiria kibaya na msingi mbaya utakaoathiri chaguzi zingine ukiwemo
wa Serikali za Mitaa wa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

No comments:
Post a Comment