Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa ambaye pia ni Mlezi wa Magereza
SACCOS Nchini akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS,
Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili kulia) alipowasili
kwenye katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma tayari kwa Mkutano Mkuu
wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi
wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unafanyika kwa siku
moja leo 30 Novemba, 2017 hapa mjini Dodoma.
Chama
cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza
Tanzania Bara (TPS SACCOS) kimefanya Mkutano wake Mkuu wa Tano wa Mwaka
2017 kwa ufanisi Mkoani Dodoma.
Mkutano
huo umefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo katika
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Miyuji Dodoma leo Novemba 30,
2017.
Akiongea
katika Mkutano huo Kaimu Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini,
Bw. Charles Malunde kwa niaba ya Naibu Mrajisi ametoa angalizo kwa
Vyama vya ushirika nchini kutokufanya biashara za Kibenki nje ya lengo
la kuanzishwa kwa SACCOS.
Amesema
kuwa katika vyama vingi vya ushirika uzoefu umeonesha kuwa wakishakuwa
na mtaji mkubwa huwa na wazo la kuanzisha Benki, ametoa angalizo kuwa
masharti ya uendeshaji wa Benki ni tofauti kabisa na masharti ya
uendeshaji wa vyama vya ushirika hivyo ameziasa Saccos zote nchini
kutafakari vyema kabla ya kubadili vyama hivyo na kuwa Benki.
“
Ukianzisha Benki huduma za Saccos zitafifia, kumbukeni wateja wa Saccos
ni pamoja na wale wa hali ya chini kabisa ikiwa benki hawa huenda
mkawaacha” alisisitiza Kaimu Mrajis Malunde.
Aidha,
amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli
zake kwa kufuata sheria lakini pia kuheshimu na kusikiliza sana wenye
mali ambao ni wanachama wa vyama hivyo vya ushirika.
Aliongeza
kuwa kwakuwa Mkutano huu utahusisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi Bw.
Charles Malunde pia amewaasa Wajumbe wa Mkutano Mkuu kuwa makini katika
uchaguzi huo kwa kuchagua watu wenye weledi na wenye mapenzi ya dhati na
ushiriki wao ili waweze kutimiza majukumu yanayokusudiwa.
Pia
amewataka wagombea wote wanaowania nafasi mbalimbali za chama hicho
kujiuliza mambo manne kama ifuatavyo;- Je, watumishi wa Jeshi la
Magereza wote ni wanachama? na mnaweka Mkakati gani?, Je wanachama
wanaweka akiba za kila mwezi?, Mnajiendesha kisayansi? Mtu akitaka mkopo
anapata baada ya muda gani? na swali la mwisho uhusiano na vyama
vingine vya ushiriki, SCULT, nje ya nchi ukoje?.
Awali
akitoa taarifa ya Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi
wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS), Mwenyeki wa Bodi ya
Magereza Saccos, DCP. Gideon Nkana amesema kuwa Idadi ya wanachama
imeongezeka hadi kufikia wanachama zaidi ya 13,000 ikiwa na mtaji wa
zaidi ya bilioni 18.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon
Nkana(katikati) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(kushoto) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS kuingia Ukumbini
tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba
na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(kulia) ni
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana
akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo
cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika
Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma..
Kaimu
Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde akitoa
hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha
Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania
Bara.
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na
Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakisikiliza
hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha.
Mjumbe
wa Mkutano huo ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Naibu
Kamishna wa Magereza, Jeremiah Nkondo akichangia mada katika Mkutano
Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha
Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara .
Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiteta jambo na Mgeni rasmi
Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde
kama inavyoonekana katika picha.
Kaimu
Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles
Malunde(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya
Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza
Tanzania Bara(waliosimama). Walioketi(wa tatu toka kushoto) ni Kamishna
Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos anayemaliza muda wake, Naibu
Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili toka kushoto) ni Kamishna wa
Fedha na Utawala, Gaston Sanga mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa
Tano unaofanyika kwa siku moja Mkoani Dodoma(Picha zote na Kitengo cha
Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza
No comments:
Post a Comment