Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
asubuhi tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya
ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya
Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan
ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson
Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi
Chana.
Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Nairobi
Tuesday, 28 November 2017
Home
KIMATAIFA
Makamu wa Rais wa tanzania alivyowasili kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa KENYA
Makamu wa Rais wa tanzania alivyowasili kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa KENYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment