Rais muapishwa wa Kenya Uhuru Kenyatta
ametangaza neema kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa
kuruhusu kuingia nchini humo kwa kutumia kitambulisho cha taifa tu na
kupewa haki zingine kama raia wa Kenya.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Rais Uhuru
Kenyatta alipokuwa akilihutubia taifa mara baada ya kuapishwa , na
kusema kwamba raia wa Afrika Mashariki watahudumiwa kama raia wa Kenya
na kupewa haki zote za msingi ikiwemo kufanya kazi nchini humo, huku
wale wa nchi zingine za Afrika watapewa viza akifika katika kiingilio
chochote mpakani au viwanja vya ndege Kenya.
Pamoja na hayo Uhuru Kenyatta amesema
hataweka masharti kwamba lazima mataifa mengine yafanye hivyo kwa
wakenya watakaotaka kuingia kwenye nchi zao.
No comments:
Post a Comment