Uongozi
wa klabu kongwe ya Yanga, umekiri kuwa kipa wa timu hiyo, Beno
Kakolanya anawadai fedha za usajili na si yeye pekee bali ni wachezaji
wengi wanaidai klabu hiyo, hivyo awe na subira.
Hivi
karibuni kumekuwa na taarifa kuwa kipa huyo huenda akatimka ndani ya
klabu hiyo baada ya klabu kushindwa kulipwa fedha zake za usajili kwa
wakati.
Kipa
huyo alijiunga na Yanga akitokea Tanzania Prisons kwa mkataba wa miaka
miwili na mkataba huo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Katibu
wa timu hiyo, Boniface Mkwasa amesema madai ni jambo la kawaida kwa
klabu yoyote, hivyo wachezaji wanatakiwa kuwa na subira, kila kitu
kitawekwa sawa.
"Ni
kweli Beno anatudai fedha zake za usajili lakini siyo yeye peke yake,
wapo wachezaji wengi ambao wanaidai klabu na wakati ukifika watapewa
fedha zao, cha msingi ni kuwa na subira.
"Mimi
nafahamu suala hilo na nimekuwa nikilishughulikia na kuna utaratibu
wake kwa sababu wachezaji wote wangekuwa wanalalamika sasa hivi,”
alisema Mkwasa.
No comments:
Post a Comment