puni
ya Bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa timu ya taifa,
Taifa Stars, wameelezea kuvutiwa na kiwango cha soka kilichoonyeshwa na
timu hiyo katika mchezo wake dhidi ya Benin.
Jumapili
iliyopita, Taifa Stars ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya taifa
ya Benin uliochezwa katika jijini la Porto-Novo nchini Benin.
Mkurugenzi
wa Masoko wa SBL, Ceaser Mloka, amesema kiwango cha Taifa Stars
kimekuwa kikiridhisha na kutia moyo tangu kampuni hiyo iingie udhamini
nayo.
Alisema ni jambo la kutia moyo kwamba tangu SBL itoe udhamini, Taifa Stars haijapoteza mechi yoyote, iwe ni nyumbani au ugenini.
“Tukirejea
kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya Benin, kama Benin wasingepata penalti
ni wazi kuwa Taifa Stars wangeibuka washindi,” alisema.
Mkurugenzi
huyo alifafanua kuwa, Taifa Stars walicheza vizuri katika mechi hiyo
pamoja na kwamba Benin wako mbele yao katika nafasi za Shirikisho la
Soka la Kimataifa (Fifa). Kwa mujibu wa viwango vya Fifa, Benin
inashikilia nafasi ya 86 huku Tanzania ikishikilia nafasi ya 136.
Ceaser
alisema kukosekana kwa wachezaji muhimu wawili wa Taifa Stars Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu kutokana na kuwa majeruhi pia kumeathiri
matokeo huku akisisitiza kuwa timu inaendelea kuimarika.
Mei,
mwaka huu, SBL iliingia mkataba wa miaka mitatu na Shirikisho la Soka
la Tanzania (TFF) wa thamani ya shilingi bilioni 2.1 ambao uliifanya
kuwa mdhamini mkuu wa Taifa Stars.
Udhamini
huo ni wa mara ya pili kwa SBL kuiunga mkono timu ya taifa baada ya
kampuni hiyo kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu ilipoidhamini
timu hiyo kati ya mwaka 2008 hadi 2011.
No comments:
Post a Comment