Kaimu Mkuurugenzi wa Kinga katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Janneth Mghamba akizungumza kwenye
maadhimisho ya mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 17 kila
mwaka. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Dkt. Hedwiga Swai.
Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga
Swai akizungumza na kinamama pamoja na wataalamu wengine wa afya katika
siku ya mtoto njiti duniani. Kulia ni Kaimu Mkuurugenzi wa Kinga katika
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Janneth Mghamba, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Uzazi na Mtoto
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Felix Bundara na Kushoto
ni Mkuu wa Idara ya Watoto, Dkt. Merry Charles.
Baadhi ya kinamama wenye watoto njiti wakiwa kwenye maadhimisho hayo leo Muhimbili.
aktari Bingwa wa Watoto, Dkt Agustino Massawe akiweka saini kuthibitisha kuukoa maisha ya watoto njiti.
Serikali
imesema imeweka mikakati endeleveu ya kupunguza vifo vya watoto njiti
kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Neema
Rusibamayila katika Siku ya Kimataifa ya Watoto Njiti ambayo
huadhimishwa kila mwaka Novemba 17.
“Tanzania
inakabiliwa na tatizo kubwa la vifo vya watoto wachanga chini ya mwezi
mmoja hivyo kutokana na hali hii tunapaswa kudhibiti vifo kwa watoto
wachanga,” alisema Dkt. Rusibamayila.
Alisema
takwimu zinaonyesha asilimia 13 hadi 17 ya watoto wote wanaozaliwa
Tanzania ni njiti na kwamba kutokana na hali hiyo Serikali kupitia
Wizara ya Afya, imekuwa ikiratibu progamu mbalimbali za kupunguza
vifo vya watoto wachanga na wa chini ya miaka mitano.
Mkurugenzi
huyo alisema moja ya program hizo ni kumsaidia mtoto kupumua baada ya
kuzaliwa, kupanua huduma za watoto wachanga kwa kujenga wodi za watoto
wachanga katika hospitali za manispaa na wilaya pamoja na kutoa mafunzo
kwa wa hudumu wa afya jinsi ya ya kuhudumia watoto wachanga.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa
Lawrence Museru alisema kuwa hospitali hiyo kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali inaendelea kutoa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa
wauguzi na madaktari wa kitengo cha watoto wachanga ili kuongeza ufanisi
wa kazi.
“Pia
tumeongeza wodi mpya ya watoto wachanga na kukarabati wodi ya za zamani
ili kutoa huduma bora kwa watoto wengi zaidi. Sambamba na kuongeza wodi
nyingine, pia tunatarajia kuzindua wodi maalumu ya watoto wachanga
mahututi (NICU) katika maadhimisho haya. Ili kutapunguza msongamano
wodini,” alisema Profesa Museru.
Profesa
Museru alisema hospitali imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma
kwa watoto wachanga kama vile kuongeza vifaa tiba katika kitengo cha
watoto wachanga zikiwamo mashine za kusaidia watoto kupumua, dawa ya
kukomaza mapafu kwa watoto njiti.
“Katika
kuadhimisha siku hii muhimu kwa watoto, Hospitali ya Taifa Muhimbili
inajivunia kuwa na wodi maalumu yenye wauguzi waliobobea kwenye kutoa
huduma na mafunzo kwa kina mama wenye watoto njiti wenye uzito wa
kuanzia gramu 500 kwa njia ya Kangaroo mother care. Nina imani kuwa
wamama wote wanaolazwa wodi ya Kangaroo ni walimu na mabalozi wazuri kwa
wa mama wenzao,” alisema Profesa Museru.
Profesa
Museru Muhimbili imefanikiwa kwa asilimia kubwa kupunguza vifo vya
watoto wachanga kutoka asilimia 19.8 mwaka 2015/2016 hadi asilimia 7.4
mwaka 2016/17.
“Idadiya
watoto waliolazwa kwenye wodi ya Kangaroo walikuwa kati ya gramu 500 na
kilo 1.5 na idadi kubwa ya watoto waliotunzwa katika wodi ya Kangaroo
waliofanikiwa kutoka wodini na uzito wa kilo 1.6 hadi 1.7 ambayo ni sawa
na asilimia 99.5 ya watoto wote waliolazwa wodi ya kangaroo.
No comments:
Post a Comment