Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki ametoa wito huo Novemba 16, 2017 Jijini Dar
es Salaam alipokutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke
na ujumbe alioambatana nao Wizarani hapo kutoka kwenye Ubalozi huo ili
kujadiliana masuala mbalimbali ya madini ikiwemo fursa za uwekezaji.
Waziri
Kairuki alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za
madini na hivyo zipo fursa lukuki za uwekezaji ambazo zinaweza kutumiwa
na kampuni za nchini China kwa manufaa ya pande zote mbili.
“Rasilimali
za madini ni nyingi na hivyo zipo fursa mbalimbali ambazo zinaweza
kutumiwa na kampuni za China na wakati huo huo kuchangia katika uchumi
na pato la Taifa kwa ujumla,” alisema Waziri Kairuki.
Waziri
Kairuki vile vile alisema yapo maeneo ambayo wawekezaji wanaweza
kushirikiana na Serikali ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni uchimbaji wa
madini kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), tafiti
za utambuzi wa maeneo yenye madini kwa kushirikiana na Wakala wa
Jiolojia Tanzania (GST) na Chuo cha Madini (MRI).
Aidha,
aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha madini yanayochimbwa
nchini yanaongezwa thamani kabla hayajasafirishwa ili kukuza uchumi wa
Taifa na wakati huo huo, kuongeza mapato ya Serikali na kuzalisha ajira
zaidi.
“Madini
yakiongezwa thamani hapa nchini, faida zitakazopatikana ni nyingi na ni
kubwa ikiwemo ajira lakini pia mapato nayo yataongezeka kwa kuelewa
thamani halisi ya madini husika,” alisema Waziri Kairuki.
Kwa upande wake Balozi Ke alipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuwaletea wananchi wake maendeleo endelevu.
Alisema
Serikali ya China itaendeleza ushirikiano wa karibu na wa dhati na
Serikali ya Tanzania hususan kwenye Sekta ya Madini ili kuhakikisha
sekta hiyo inaleta tija iliyokusudiwa kwa Taifa.
Alisema kampuni mahiri nyingi kutoka China tayari zimeonyesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini na ziko tayari kuja kuwekeza Nchini.
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akizungumza na Balozi wa China
nchini Tanzania, Wang Ke na ujumbe alioambatana nao (hawapo pichani)
walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akimsikiliza Balozi wa China nchini
Tanzania, Wang Ke alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam ili
kujadili masuala mbalimbali.
Balozi
wa China nchini Tanzania, Wang Ke (kulia) akiwa na ujumbe wake kutoka
Ubalozi wa China nchini Tanzania walipomtembelea Waziri wa Madini,
Angellah Kairuki (hayupo pichani) ili kujadili masuala mbalimbali ya
Sekta ya Madini.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (wa pili kutoka kulia) akijadiliana jambo na ujumbe kutoka Ubalozi wa China nchini ulioongozwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (katikati).
No comments:
Post a Comment