Rais Donald Trump amemwambia waziri mkuu
wa Uingereza Theresa May kuangazia ugaidi nchini Uingereza badala ya
kumkosoa kwa kusambaza video za kundi la mrengo wa kulia la Uingereza
ambalo linaeneza chuki.
''Usiniangazie sana mimi, angazia ugaidi
unaotekelezwa na makundi yalio na itikadi kali ambao unatekelezwa
nchini humo'', Trump alituma ujumbe wa Twitter.
Rais huyo wa Marekani awali alituma
video tatu zenye chuki zilizosambazwa katika mtandao wa Twitter na
makundi hayo nchini Uingereza.
Msemaji wa bi May alisema kuwa ni makosa kwa rais kufanya hivyo.
Marekani na Uingereza ni washirika wa karibu na wameelezewa kuwa na ''uhusiano maalum''.
Theresa May alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kumtembelea rais Trump katika ikulu ya Whitehouse.
Kanda za video zilizosambazwa na Trump
ambaye ana takriban wafuasi milioni 40 awali zilikuwa zimechapishwa na
Jayda Fransen, naibu kiobngozi wa kundi la Uingereza la Britain First,
kundi lililoanzishwa na wanachama wa zamani wa mrengo wa kulia wa chama
cha Uingereza cha BNP.
Bi Fransen mwenye umri wa miaka 31
ameshtakiwa nchini Uingereza mwa kutumia maneno ya kutisha, na matusi
katika hotuba alizotoa katika mkutano mjini Belfast.
Wanasiasa nchini Uingereza wameukosoa
ujumbe huo wa rais Trump akiwemo, askofu mkuu wa Cantebury Justin Welby
ambaye alisema kuwa inakera kwamba rais Trump aliamua kulipatia sauti
kundi lenye itikadi kali la mrengo wa kulia.
Hatua hiyo imezua hisia kali huku baadhi
ya raia wakitaka ziara ya rais Trump nchini Uingereza kufutiliwa mbali
,ijapokuwa afisi ya waziri mkuu imesema kuwa ziara hiyo bado itafanyika.
No comments:
Post a Comment