MBUNGE wa jimbo la Uzini kupitia tiketi
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Mfanyabiashara, Mohd Raza
amewataka wafanyabiashara nchini kushikiriki kikamilifu katika zoezi la
kulipa kodi ili kuweza kuwafikishia wananchi wa hali ya chini huduma
muhimu.
Wito huo ameutoa jijini Dar es Salaam,
Mapema leo hii wakati alipokua akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
msaada wa vifaa mbalimbali vya kuchezea mpira wa Miguu katika vyenye
thamani ya shilling million 50 kwa lengo la kutoa fursa kwa vijana
kuweza kuonesha vipaji vyao.
Amesema kuwa, Serikali ya awamu ya Tano
katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) haitomuonea yoyote
hivyo ni vyema watu wakaweka utaratibu wa kuweza kulipia kodi ili
kuweza kuwasaidia wananchi wa hali ya nchini waishio vijijini kwa
kuwasogezea huduma muhimu ikiwemo Maji,Barabara pamoja na Umeme.
"Kodi zetu ndio zinazochangia kusukuma
maendeleo vijijini , kwani bado kuna sehemu nyingi kunauhitaji mkubwa wa
huduma za kijamii ikiwemo Maji, Umeme pamoja na Barabara hivyo tuwe
tayari katika kutoa msaada wa kufikisha huduma hizi jambo ambalo
litaleta Maendeleo ya Haraka kwa wananchi husika"amesema Raza.
Aidha ameongeza kuwa,Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imekua ikifanya kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya haraka kwa
wananchi, lengo ikiwa ni kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
kama ambavyo alifanya Hayyat Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere pamoja
Mzee Abeid Aman Karume.
No comments:
Post a Comment