Kiongozi wa Upinzani Kenya NASA, Raila
Odinga amesema anatarajia kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo Desemba 12,
mwaka huu ambayo itakuwa siku ya uhuru wa Kenya.
Odinga ametoa kauli hiyo ikiwa katika
uwanja wa Jacaranda saa chache baada ya Rais Kenyatta kuapishwa kuwa
Rais katika uwanja wa Kasarani.
Hata hivyo, wakati Odinga akisema hayo,
Rais Kenyatta mara baada ya kuapa amewaambia na wananchi wa Kenya kuwa
hakutakuwa na shughuli zingine za uchaguzi na yeye ndiye Rais mteule wa
Kenya.
Hata hivyo, Polisi nchini Kenya
walivamia uwanja uliopangwa kufanyika mkutano na maombolezo ya wananchi
waliofariki wakati wa vurugu za uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba
26, mwaka huu.
Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa leo kuwa Rais wa Kenya ili kuwatumikia wakenya katika muhula wa pili wa uongozi.
No comments:
Post a Comment