Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa Vifaa mbalimbali vya
michezo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Uzini,Zanzibar Muhammed Hussam
Raza kwa ajili ya mashindano ya majimbo yatakayofanyika Jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake mapema hii Leo jijini Dar es Salaam Wazir Majaliwa wakati
wa kupokea vifaa hivyo vyenye thamani ya fedha taslimu Milioni 50,
amesema vifaa hivyo Vitagawiwa kwa majimbo 10 katika wilaya zote za
mkoa wa Dar es.
Amesema kuwa,ni vyema mashindano hayo
yakaanza haraka huku akisisitiza kufuatwa kwa taratibu zote za Fifa ili
kuweza kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa mashindano ikiwa nipamoja na
vijana kuweza kuonesha vipaji vyao na kutoa fursa mbalimbali na
kufahamiana na hata kuwa na mpango endelevu wa michezo.
"Mashindano hayo yaanze mapema ipasavyo
bila kusahau kutekeleza tija na malengo ya mashindano hayo kwani
kupitia mashindano hayo tunaweza kupata wachezaji ambao wanaweza kuunda
team ya Taifa" alisema Majaliwa.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la
Uzini, Visiwani Zanzibar Muhammed Hassam Raza amesema kuwa ametoa msaada
huu kwa lengo la kuhakikisha michezo inakuwa ndani ya mkoa wa Dar es
salaam, pamoja na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.
Amesema kuwa, katika mashindano hayo
kutokua na Zawadi mbalimbali kwa washiriki katika majimbo ikiwa ni
pamoja na jezi, viatu, mipira na gloves kwa magolikipa,pia ameweza
kutoa zawadi vya vifaa vya michezo kwa ofisi ya waziri mkuu pamoja na
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Ofisi ya Chama cha Mapinduzi pakoja na
Marefa watakaosimakia vizurinmashindano hayo.
No comments:
Post a Comment