Samatta aanza kupata ahueni - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday 15 November 2017

Samatta aanza kupata ahueni

Samatta aanza kupata ahueni

Mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta ameanza kutembea hata bila ya kutumia magongo.
Samatta ni majeruhi na amefanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni.

Nahodha huyo wa Taifa Stars, aliumia wakatri akiitumikia Genk katika mechi dhidi Lokeren na kutolewa nje katika dakika ya 40.

Lakini Samatta leo ametupia picha akijaribu kutembea bila ya kutumia magongo maalum ambayo alionekana akiyatumia siku tatu zilizopita.

Jana alionekana akiwa ameanza mazoezi na leo amejaribu kutembea bila ya magongo jambo ambalo linaleta faraja kuwa atapona mapema.

Kwani kitengo cha madaktari wa Genk ambacho kinasifika kwa huduma nzuri kimemtaka Samatta kukaa nje hadi wiki sita akiendelea na matibabu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here