Baada ya kuwepo kwa taarifa za kuhojiwa
kwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenga, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera,
Severine Niwemugizi (61) na Idara ya Uhamiaji kuhusu uraia wake, Mbunge
wa Tarime Vijijini, John Heche amesema utawala wa Rais Kikwete,
makanisa yalisimama na kukosoa.
Heche amesema kwamba utawala wa Kikwete
Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo kadhaa wakati ya serikali na wala
hakuwahi kushuhudia viongozi wa dini wakihojiwa na kusisitiza kwamba
watu wasimame imara kupinga kuporwa kwa uhuru.
"Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo
kadhaa wakati wa utawala wa Kikwete, sikuona kiongozi anahojiwa uraia
wake naamini ingekuwa kipindi hiki kanisa lingefutwa wangesema sio
kanisa la Kitanzania, tusimame imara kupinga uhuru wetu kuporwa, hakuna
alie salama" Heche.
Taarifa zinadai kwamba Askofu Niwemugizi
alihojiwa mara 2 na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na Uraia wake kati ya
mwezi Novemba na Disemba.
Mwishoni mwa mwezi Septemba , Askofu
Niwemugizi alisema kuwa imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira
nzuri ambayo pia italetwa na Katiba Mpya.
No comments:
Post a Comment