Baada ya Askofu wa katoliki kuhojiwa, Mbunge wa Chadema amfungukia haya JK. - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Tuesday, 12 December 2017

Baada ya Askofu wa katoliki kuhojiwa, Mbunge wa Chadema amfungukia haya JK.

Baada ya kuwepo kwa taarifa za kuhojiwa kwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenga, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61) na Idara ya Uhamiaji kuhusu uraia wake, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amesema utawala wa Rais Kikwete,

makanisa yalisimama na kukosoa.
Heche amesema kwamba utawala wa Kikwete Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo kadhaa wakati ya serikali na wala hakuwahi kushuhudia viongozi wa dini wakihojiwa na kusisitiza kwamba watu wasimame imara kupinga kuporwa kwa uhuru.

"Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo kadhaa wakati wa utawala wa Kikwete, sikuona kiongozi anahojiwa uraia wake naamini ingekuwa kipindi hiki kanisa lingefutwa wangesema sio kanisa la Kitanzania, tusimame imara kupinga uhuru wetu kuporwa, hakuna alie salama" Heche.

Taarifa zinadai kwamba Askofu Niwemugizi alihojiwa mara 2 na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na Uraia wake kati ya mwezi Novemba na Disemba. 

Mwishoni mwa mwezi Septemba , Askofu Niwemugizi alisema kuwa  imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri ambayo pia italetwa na Katiba Mpya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here