MO IBRAHIM, SIMBA MAMBO SAAFI SASA HAKUNA MATATA YA MKATABA - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Tuesday, 12 December 2017

MO IBRAHIM, SIMBA MAMBO SAAFI SASA HAKUNA MATATA YA MKATABA

Klabu ya Simba imemalizana na mchezaji wake Mohamed Ibrahim na kukubaliana kumuongezea mkataba.
Ibrahim maarufu kama Mo Ibrahim, alitarajia kuongeza mkataba leo mchana.

“Ilikuwa ni leo mchana, sijajua imekuwaje lakini kila kitu kimemalizika na makubaliano ya kila kitu yameenda vizuri.

“Suala la kusaini mkataba ndiyo lilibaki na sasa hakuna hofu tena,” kilieleza chanzo.


Kumekuwa na taarifa kwamba, Mo Ibrahim anaweza kuondoka Simba, ikiwa ni baada ya mkataba wake kwisha.
MO IBRAHIM, SIMBA MAMBO SAAFI SASA HAKUNA MATATA YA MKATABA

No comments:

Post a Comment