Na Mwandishi Maalum
MKURUGENZI
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani
alisema chama cha siasa kutangaza kugomea kushiriki uchaguzi hakuwezi
kuifanya tume ihahirishe uchaguzi kwani tume haiko kumshawishi mtu au
chama kushiriki uchaguzi.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Ramadhani alisema chama kushiriki uchaguzi
ni jambo la hiyari na tume ya uchaguzi iko pale kwa ajili ya kuweka na
kutengeza mazingira yatakayofanya vyama vya siasa kushirki uchaguzi.
Alisema
iwapo kuna chama kitaamua kutoshiriki uchaguzi, chama kitakachoshiriki
hata kama ni mmoja mgombea wake atapita bila kupingwa. Alisistiza kuwa
hakuna sehemu yoyote ya katiba na sheria ya uchaguzi inayotamka kwamba
chama kisiposhiriki uchaguzi basi uchaguzi unaahirishwa.
“Ila
ikitokea vyama vikasusa vyote kushiriki kwenye uchaguzi hapo ndipo
unaweza kuahirishwa kwa kuwa hakutakuwa na mgombea,”alifafanua
mkurugenzi wakati alipokuwa anazungumza na baadhi ya waandishi wa habari
ambao walitaka kupata ufafanuzi wa tume kuhusu tamko lililotolewea na
mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe.
Hivyo
ameviasa vyama vya siasa vinavyotishia kutoshiriki kwenye uchaguzi
mdogo wa ubunge katika majimbo matatu na kata sita kufuata mifumo ya
kisheria ya kushughulikia malalamiko ya uchaguzi.
Aliitaja
mifumo hiyo kuwa ni kuwasilisha malalamiko kwenye kamati ya maadili
wakati wa kampeni, wakati wa kuanza kupiga kura wakala akiwa na
malalamiko anajaza fomu namba 14 na fomu namba 16 wakati upigaji kura
unapoeendelea na kama mgombea hakuridhikai anaruhusiwa kwenda
mahakamani.
Juzi
Mbowe alitishia kuwa vyama vinavyounda umoja wa katiba (UKAWA)
havitashiriki uchaguzi iwapo changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati
wa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 zisipofanyiwa kazi na NEC.
Akizungumzia
hoja hiyo Ramadhani alisema kwamba katika orodha ya vyama vilivyopo
NEC, Ukawa sio moja ya vyama vya siasa na akaongeza kuwa kushiriki
kwenye uchaguzi ni hiyari ya chama cha siasa.
“Niwasihi
vyama vya siasa watumie mifumo iliyopo ya kawaida ya kuwasilisha
malalamiko yao, kwenye kamati za maadili, kujaza fomu namba 14 kabla ya
kura kuanza kupigwa, fomu 16 wakati kura zinapigwa na kuwasilisha
malalamiko mahakamani baada ya kura kuhesabiwa,”alisema Kailima.
Aliseima
hiyo ndio mifumo iliyowekwa kisheria katika kushughulikia changamoto
za uchaguzi zinapojitokeza, “Je hiyo mifumo wanayotaka wao ni ipi?
Kama kama kuna mgombea hakuridhika mahakama zipo aende maana wamepewa
siku 30 za kufungua kesi.”
Alisema
NEC haiwezi kuahirisha uchaguzi kwani sheria inatamka kuwa uchaguzi
unaweza kuahirishwa iwapo tu kuna mgombea amefariki, kutokuwepo mgombea,
zikitokea ghasia na fujo au wagombea wakifungana kwa kura.
“Je
kuna mgombea amefariki? Haya mambo yote manne hayajatokea, sasa
tutaahirishaje uchaguzi? Alihoji Ramadhani na akavitaka vyama vya siasa
kutumia mifumo iliyopo kuwasilisha malalamiko yao
Akizungumzia
kuhusu jimbo la Longido ambalo Mbowe alidai kuwa shauri la uchaguzi
bado liko mahakamani na kwamba wameiandikia NEC kuhusu suala hilo na
hawajajibiwa barua yao, Ramadhani alisema madai hayo sio ya kweli kwani
barua zote walizoandikiwa wamezijibu.
Alisema
jimbo hilo liko wazi kwa kuwa mahakama ndio imeiandikia NEC kuitaarifu
kumalizika kwa kesi iliyokuwepo mahakamani. Alisema kwamba NEC
itasimamisha uchaguzi wa jimbo hilo iwapo tu wataambiwa na mahakama
kusimamisha mchakato huo.
No comments:
Post a Comment