
SIKU chache baada ya kampuni ya udalali ya Nkaya kulalamika kuipiga mnada kinyemela nyumba moja iliyopo Mtaa wa Kondo, Kata ya Kunduchi wilayani Kinondoni, mmiliki wa nyumba hiyo Bi Benadeta Rweyendere ameibuka na kumuomba Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingilia kati.
Bi.Bernadetha Rweyendere
Mjane mwenye nyumba iliyopigwa Mnada Ndani ya Dakika Tano
Nyumba hiyo iliyopo Kitalu namba 239, T 110335, Block B, imeuzwa jana na watu waliodai ni kutoka kampuni ya udalali ya Nkaya Company Limited, huku ikiwa na pingamizi la Mahakama Kuu ya Tanzania .
Nyumba iliyopigwa Mnada ndani ya Dakika Tano
Wauzaji hao pia wamebainika kughushi saini ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo kuthibitisha kununuliwa na mmliki mpya ambaye ni Aisha Amour.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, mmiliki wa nyumba hiyo Bi. Benadeta Rweyendera amewaambia waandushi wa habari kuwa nyumba iliyopigwa mnada na Nkaya si mali ya mdaiwa Zainabu Juma Kiswaka.
Ameeleza kwamba alinunua eneo kwa Bi. Zainabu mwenye ambae ana mgogoro na Nkaya, mwaka 2015 kabla ya mgogoro huo.
Bi.Zainabu
Aliemuuzia nyumba
Amefafanua kuwa eneo hilo limekatwa katikati ambapo upande mmoja unamilikiwa na Zainabu na upande mwingine ni wake.
"Nilijenga nyumba yangu hapo kisha tulitenganisha maeneo kwa ukuta.Upande wangu na wa Zainabu. Ajabu watu wa Nkaya wamepauza pote pamoja na nyumba yangu ambayo haihusiki,"alisema Bi....
Alisema yeye nu mjane mwenye watoto watatu na tayari Nkaya wamempa notice ya siku 30 kuhama kwa sababu nyumba hiyo imeuzwa.
Awali Bi Zainabu Kiswaka alielezea kusikitishwa na tukio hilo na kwamba nyumba imeuzwa wakati kesi bado ipo mahakamani, huku pingamizi likiwa limewekwa toka mwaka 2017.
“Hati yangu ya eneo ilitumiwa na mataperi walighushi sahihi yangu na kukopea fedha benki ya KCB zaidi y ash.bilioni 1.6, kesi iko mahakamani nashangaa leo wanakuja kuuza nyumba. Naomba serikali inisaidie,”aslisema Zainabu.
Kwa mujibu wa shuhuda, Shaban Mwanga, alisema mnada umefanyika ndani ya dakika tano tu na uongozi wa serikali ya mtaa haukuhusika.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kondo , Hamis Ndonga, alithibitisha kufanyika tukio hilo ambalo alidai ni utaperi wa wazi.
Alisema wahusika wa kampuni ya Nkaya Company Limited wameghushi saini yake kuthibitisha uuzwaji wa nyumba wakati yeye hakuwepo hata kwenye eneo la tukio.
“Mimi sikuwepo hata katika eneo la tukio ingawa waliniletea hati ya kunijulisha kwamba wanafanya mnada wa nyumba hiyo. Nilisaini hati hiyo kuthibitisha kuipokea tu. Lakini sikuwa ofisini kwa sababu leo (jana) ilikuwa siyo siku ya kazi. Tena nilishangaa kuona wanafanya mnada siku ambayo si yakazi,”alisema mwenyekiti huyo.
Hata Moja ya Gazeti la chama Nchini Tanzania (Uhuru) limtafuta kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Nkaya, Hassan Magogo, ambaye alithibitisha kuuzwa kwa nyumba hiyo.
Alisema pingamizi lililokuwa limewekwa na mahakama lilikuwa limepitwa na wakati kwani ni la Mei 7 mwaka 2017.
“Kuhusu kughushi sahihi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, sheria na vyombo vya sheria vipo,”alisema mtu huyo.
Kuhusu kuuzwa kwa nyumba hiyo siku ambayo si ya kazi, Magogo , alisema mnada unaweza kufanyika siku yoyote, hata ikiwa jumamosi.
“Kama unataka njoo ofisini,”alisema.
Kati ya hati iliyotolewa na Ngaya kuhusu sababu za kuuzwa kwa nyumba hiyo, ilieleza kuwa imepewa idhini na benki ya KCB Bank Tanzania kuuza nyumba hiyo, kwa madai iliwekewa dhamana kwaajili ya kupata mkopo ambapo Zainabu alishindwa kurejesha sehemu ya mkopo huo.
Hati hiyo ilieleza kuwa mmiliki wa sasa ni Aisha Amour ambaye inadaiwa alinunua kwa mnada nyumba hiyo.
No comments:
Post a Comment