NAIBU
Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akisalimiana na sehemu ya wakulima
wa chai alipowasili kwenye kijiji cha Lwangu Wilaya ya njombe mkoani
Njombe kwa ziara ya kikazi hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Njombe, Mhe. Ruth Msafiri. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
Sehemu ya wakulima wa chai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipozungumza nao.
Sehemu
ya wakulima wa chai wakikusanya zao hilo baada ya kutoka kuvuna wakati
Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipofanya ziara na
kuzungumza nao.
NAIBU
Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea na wakulima wa chai
alipotembelea kijiji cha Lwangu Mkoa wa Njombe hivi karibuni. 
Sehemu
ya wakulima wa chai wakimpongeza Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary
Mwanjelwa alipofanya nao mazungumzo wakati wa ziara yake kwa wakulima
hao.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa akimwagiza Meneja Mkuu wa Njombe
Outgrowers Services Company (NOSC), Fibert Kavia (kushoto) kuhakikisha
risiti zao zinaonyesha kiasi cha fedha mkulima wa chai anachotakiwa
kulipwa baada ya kupima bidhaa hiyo wakati kuuza zao hilo kwa kampuni
hiyo. Wanaosikiliza (wa pili kushoto) ni Mkulima wa chai iliyopimwa,
Juliana Casian na Karani wa NOSC, Flora Sanga.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa (wa pili kushoto) akiangali kitalu
cha mbegu za kupandikizwa za maparachichi alipofanya ziara na
kuzungumza na wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Nundu, Wilaya ya
Njombe Mkoani Njombe. Kushoto ni Afisa Kilimo wa Wakulima wa zao hilo,
Damasi Kasalala, Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo na
ujumbe wa viongozi wa serikali.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa akipata maelezo ya mche
uliopandikizwa wa parachichi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT,
Geoffrey Kirenga (kulia) na Afisa Kilimo, Damasi Kasalala alipofanya
ziara na kuzungumza nao wakulima wa zao hilo. Kushoto ni Mbunge wa jimbo
la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo.
Wataalamu
wa kuandaa mbegu za parachichi, Henry Mwepel (kulia), na Lugano Mwalusi
wakifanya upandikizaji wa miche ya parachichi kutoka ule wa asili kuwa
wa kisasa katika kitalu maalumu cha uzalishali wa zao.
NAIBU
Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akilakiwa na wakulima wa viazi
mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe
mkoani Njombe, alipowatembelea na kuzungumza nao kujua changamoto zao na
kutoa ushauri wake kukabiliana nazo. Pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya
Njombe, Mhe. Ruth Msafiri.
Wakulima
wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya
Njombe mkoani Njombe, wakimpokea kwa furaha Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.
Dk. Mary Mwanjelwa.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa akiwasabahi wakulima wa viazi
mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe
mkoani Njombe alifanya ziara mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (kulia) Mbunge wa jimbo la
Njombe, Mhe. Edward Mwalongo (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa
SAGCOT, Geoffrey Kirenga wakifuatilia jambo Mhe. Mwanjelwa alipozungumza
na wakulima hao.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akipata maelezo
kutoka kwa Mwenyekiti wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kukusanya,
kuchambua, kufungasha na kuuzia viazi mviringo kijiji cha Lusitu, namna
bora ya uzalishaji wa viazi wakati Mhe. Mwanjelwa alipofanya ziara na
kufanya nao mazungumzo.
No comments:
Post a Comment