JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI Mkurugenzi Mkuu mpya wa KAMPUNI ya Jumia Tanzania,Zadok Prescott akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,alipokuwa akijitambulisha na kueleza mikakati mipya ya kuiendelea kampuni hiyo amayo kwa sasa imezidi kutanuka kila kukicha,kushoto kwake ni Meneja Masoko Albanny Jamess Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albanny Jamess akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,kuhusu ujio wa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo,na kuelezea namna Jumia ilivyodhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko. Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii KAMPUNI ya Jumia Tanzania inayojishughulisha na huduma za uuzaji na manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa njia mtandao imemtambulisha Zadok Prescott kuwa Mkurugenzi Mkuu wake mpya. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho wake uliofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Prescott alibainisha ni fursa kwake kujiunga na kampuni hiyo. Ambapo amesema Jumia ni kampuni ambayo imedhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko. “Jumia ilianzishwa mnamo mwaka 2012 ikiwa na imani thabiti ya kwamba: ‘Mtandao wa intaneti unaweza kuboresha maisha ya Waafrika.’ "Ni vigumu kupata bidhaa unayoihitaji kupitia mfumo wa sasa wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali Tanzania. " Upatikanaji wa bidhaa katika sehemu tofauti huwalazimu wateja kusafiri umbali mrefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kuongezea, bei hutofautiana kwa kila mfanyabiashara jambo linalosababisha kuwa ni changamoto kutambua kama unauziwa bidhaa kwa bei sahihi au la,"amesema. Ameongeza ni mfumo ambao humpotezea mteja muda na gharama katika maisha yake ya kila siku. Hivyo dhumuni kubwa la Jumia ni kuufanyia mabadiliko mfumo huo na kuufanya uwe wenye tija kwa wafanyabiashara nchini na kuwapatia wigo zaidi,” alisema Prescott. Akifafanua namna Jumia ilivyodhamiria kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara nchini ameelezea wafanyabiashara wanakumbwa na changamoto lukuki katika uendeshaji wa biashara zao. Ametaja baadhi yake ni gharama kubwa za pango hususani kwenye maeneo yenye wateja wengi. "Hali hii husababisha wafanyabiashara wengi kuwa na idadi ya wateja walewale kulingana na eneo walilopo,” amesema na kuongezea, “Ili kuwafikia wateja kuwajulisha kuhusu biashara zao, inamlamzimu mfanyabiashara kufanya matangazo na kutafuta masoko, jambo ambalo ni gharama kubwa na sio wote wanakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.” Amefafanua Jumia ndio suluhu pekee kwa wateja na wafanyabiashara kwani imekusanya bidhaa za aina tofauti sehemu moja, ikitoa bei zenye ushindani, pamoja na kumfikishia mteja popote alipo kwa urahisi. Amesema mteja anaweza kufanya manunuzi mwenyewe kwa kuingia kwenye mtandao wao, akachagua bidhaa azipendazo na kisha akapelekewe mpaka alipo baada ya kuagiza. " Katika kujenga uaminifu kwa wateja wetu, malipo hufanyika baada ya kumfikia mteja. Kwa kuongezea, mteja huwa hadaiwi malipo pindi asiporidhika na bidhaa aliyopelekewa au akitaka ifanyiwe mabadiliko. "Hivyo, tunawaahidi wateja wetu bidhaa nyingi zaidi kukidhi mahitaji yao, bei zenye ushindani zaidi na kuwafikishia bidhaa popote walipo kwa haraka, urahisi na gharama nafuu,” ameongezea. Amesema zaidi ya kampuni 50,000 za kiafrika zinauza bidhaa zake kupitia Jumia kila siku na kwamba wanafanya jitihada za kuhamisha shughuli za kiuchumi kwenda mtandaoni Na kuziwezesha kampuni za Kiafrika ndogo, za kati na kubwa kupata wateja wapya na kuwahudumia kwa mbinu mpya. " Takribani wajasiriamali na wafanyabiashara 50,000 wanauza bidhaa zao kupitia Jumia, zaidi ya bidhaa 10,000 zinajitangaza kupitia Jumia. "Pia kampuni kadhaa za usafirishaji husafirishaji mamilioni ya bidhaa kila mwaka kwa sababu ya Jumia. Kila siku, tunasaidia na kuhamasisha migahawa, hoteli, wafanyabiashara wadogo, bidhaa, mawakala wa makazi na usafiri, "Makampuni makubwa, kampuni za usafirishaji kuwa bora na kubwa, kwa kutumia msaada wa ripoti za tafiti mbalimbali kuzisaidia kuwa bora na kutoa huduma nzuri kwa wateja," amesema . Ameongeza wanaamini kupitia hivyo wataleta mabadiliko chanya barani Afrika. Prescott amesema mojawapo ya fursa ambayo wafanyabiashara wengi wa kitanzania bado hawajaigundua ni namna ya kuwafikia wateja wanaopatikana mtandaoni. Ambapo amesema ni kwa kujiunga na Jumia, watawapatia fursa ya kukuunganisha na mamilioni ya wateja waliopo mtandaoni. " Tunaweza kumuwezesha mfanyabiashara mdogo anayefanya shughuli zake kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam kuuza bidhaa zake kwa wateja walioko Tanzania nzima. "Tunazitangaza bidhaa tofauti kwa kuziwezesha kuonekana kwa mtu yeyote aliyeunganishwa na mtandao wa intaneti,” amesema. Mkurugenzi Mkuu huyo mpya wa Jumia nchini Tanzania,amesema “wafanyabiashara wanaojiunga nasi hawana haja ya kugharamia shughuli za kutafuta masoko au kukodisha maduka kwa gharama kubwa. "Hii ni huduma ambayo Jumia huitoa kwa kamisheni nafuu kupitia mauzo yatakayofanyika mtandaoni. Kitu pekee tunachokihitaji kutoka kwao ni kuuza bidhaa zenye ubora na bei nafuu kwa wateja wetu.” Katika jitihada za kujenga hamasa ya biashara mtandaoni, Jumia huandaa shughuli za mara kwa mara za kimasoko ndani ya mwaka kama vile kuzindua bidhaa mpya, ofa kabambe na mapunguzo lukuki kwa ajili ya wateja. Kwa upande wake Mkuu wa Masoko wa Jumia Tanzania, Albany James alipata fursa ya kugusia juu ya Jumia kuzindua kwa mara ya kwanza ‘Wiki ya Simu,’ kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Tigo. Ameelezea kampeni hiyo inafanana na kampeni yao ya kila mwaka ya ‘Black Friday,’ lakini hiyo itajikita kwenye bidhaa za simu za mkononi pekee. "Kampeni hii itahusisha uzinduzi wa bidhaa mpya, ofa kabambe, zawadi na punguzo kwa wateja. Tukio hili tayari limekwishafanyika kwenye nchi za Kenya na Nigeria ambapo ni kubwa na maarufu, na kwa mara ya kwanza watanzania watanufaika na mapunguzo ya kuvutia na promosheni zitakazoletwa kwa ajili yao na Jumia. "Itakuwa ni wiki ya aina yake kwa ajili ya kununua bidhaa za simu.Wiki ya Simu’ itaanza Machi 19 mpaka Machi 25 mwaka huu ambapo itazinduliwa kwa muda wa siku mbili, Machi 17 & 18 katika viwanja vya Leaders Club," amesema. Ameongeza uzinduzi huo utazileta pamoja kampuni mbalimbali maarufu za simu nchini katika tukio ambalo litakuwa ni la kipekee, la kifamilia, ambapo wahudhuriaji watakuwa na mazingira mazuri ya kununua bidhaa za simu na kufurahia chakula na muziki mzuri kwa ajili yao. "Tukio hili litawapatia wateja fursa ya kununua na kujionea matoleo mapya ya bidhaa za simu ambazo zinatawala soko kwa sasa kwa gharama nafuu pamoja na kujifunza mambo mengi zaidi kuhusu Jumia,” ameelezea James. Akijaribu kufafanua kwa kifupi kuhusu bidhaa na ofa zitakazokuwepo kwenye ‘Wiki ya Simu,’ Mkuu huyo wa Masoko amesema Jumia kwa kushirikiana na Tigo, zimekuwa ndiyo kampuni za kwanza kuwapatia wateja fursa ya kuagiza simu ya Samsung S9 na S9+ kabla haijaingia sokoni. " Mchakato wa kuagiza Samsung S9 lilianza mara moja kupitia Jumia mara baada ya hafla ya uzinduzi wa simu hiyo kufanyika kwa njia ya mtandao duniani kote kutoka kwenye Mkutano wa Dunia wa Simu za mkononi uliofanyika jijini Barcelona, Hispania Februari 25 mwaka huu. “Wateja watakaoagiza kupitia mtandao wa Jumia wataweza kujipatia simu zao wiki moja kabla ya Wiki ya kampeni, na watapokea kifaa cha kuchaji kwa haraka kinachotumia waya na miezi 6 ya bure ya kuunganishwa na intaneti kutoka Tigo,"amesema. Amefafanua vilevile watakuwa na zawadi za kushtukiza siku ya tukio, katika wiki hiyo wateja wao watapatiwa ‘chemsha bongo’ ya kuitafuta simu ya Samsung S9 yenye thamani ya zaidi ya milioni 2, Amesena ambayo itakuwa imefichwa kwenye mtandao wao kwa kununua bidhaa zenye gharama isiyopungua Sh. 100,000 " Mteja wa kwanza kuivumbua ataweza kujipatia simu hiyo kwa gharama nafuu zaidi nchini. Tutakuwa na ofa za kuvutia, vocha na mapunguzo ambavyo vitawekwa wazi kadri tutakavyokaribia uzinduzi wa wiki hiyo,” amesema James. Kabla ya kujiunga na Jumia Tanzania, Zadok Prescott alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Millicom (kampuni mama ya Tigo na Zantel) katika kitengo cha Kutafuta na Kuunganishaji biashara mpya kuanzia mwaka 2014 mpaka 2018. Prescott anao uzoefu mkubwa katika masuala ya ushauri wa mikakati, utafutaji na uunganishaji wa biashara mpya, kuboresha biashara, ambapo uzoefu wake unatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kupelekea Jumia kuwa mojawapo ya kampuni inayoongoza kwenye utoaji wa za huduma za biashara mtandaoni nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla. Posted by MICHUZI BLOG at Thursday, March 01, 2018 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest DK MWAJELWA AWAPONGEZA WAKULIMA WA CHAI NA PARACHICHI MKOA WA NJOMBE NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akisalimiana na sehemu ya wakulima wa chai alipowasili kwenye kijiji cha Lwangu Wilaya ya njombe mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Ruth Msafiri. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) Sehemu ya wakulima wa chai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipozungumza nao. Sehemu ya wakulima wa chai wakikusanya zao hilo baada ya kutoka kuvuna wakati Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipofanya ziara na kuzungumza nao. NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea na wakulima wa chai alipotembelea kijiji cha Lwangu Mkoa wa Njombe hivi karibuni. Sehemu ya wakulima wa chai wakimpongeza Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipofanya nao mazungumzo wakati wa ziara yake kwa wakulima hao. Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa akimwagiza Meneja Mkuu wa Njombe Outgrowers Services Company (NOSC), Fibert Kavia (kushoto) kuhakikisha risiti zao zinaonyesha kiasi cha fedha mkulima wa chai anachotakiwa kulipwa baada ya kupima bidhaa hiyo wakati kuuza zao hilo kwa kampuni hiyo. Wanaosikiliza (wa pili kushoto) ni Mkulima wa chai iliyopimwa, Juliana Casian na Karani wa NOSC, Flora Sanga. Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa (wa pili kushoto) akiangali kitalu cha mbegu za kupandikizwa za maparachichi alipofanya ziara na kuzungumza na wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Nundu, Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe. Kushoto ni Afisa Kilimo wa Wakulima wa zao hilo, Damasi Kasalala, Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo na ujumbe wa viongozi wa serikali. Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa akipata maelezo ya mche uliopandikizwa wa parachichi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga (kulia) na Afisa Kilimo, Damasi Kasalala alipofanya ziara na kuzungumza nao wakulima wa zao hilo. Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo. Wataalamu wa kuandaa mbegu za parachichi, Henry Mwepel (kulia), na Lugano Mwalusi wakifanya upandikizaji wa miche ya parachichi kutoka ule wa asili kuwa wa kisasa katika kitalu maalumu cha uzalishali wa zao. NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akilakiwa na wakulima wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe mkoani Njombe, alipowatembelea na kuzungumza nao kujua changamoto zao na kutoa ushauri wake kukabiliana nazo. Pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Ruth Msafiri. Wakulima wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe mkoani Njombe, wakimpokea kwa furaha Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa. Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa akiwasabahi wakulima wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe mkoani Njombe alifanya ziara mkoani humo. Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (kulia) Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga wakifuatilia jambo Mhe. Mwanjelwa alipozungumza na wakulima hao. Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kukusanya, kuchambua, kufungasha na kuuzia viazi mviringo kijiji cha Lusitu, namna bora ya uzalishaji wa viazi wakati Mhe. Mwanjelwa alipofanya ziara na kufanya nao mazungumzo. Posted by MICHUZI BLOG at Thursday, March 01, 2018 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Older Posts Home Subscribe to: Posts (Atom) - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

Thursday, 1 March 2018

JUMIA TANZANIA YAAHIDI KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA, MAMILIONI YA WATEJA WALIOKO MTANDAONI Mkurugenzi Mkuu mpya wa KAMPUNI ya Jumia Tanzania,Zadok Prescott akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,alipokuwa akijitambulisha na kueleza mikakati mipya ya kuiendelea kampuni hiyo amayo kwa sasa imezidi kutanuka kila kukicha,kushoto kwake ni Meneja Masoko Albanny Jamess Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albanny Jamess akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,kuhusu ujio wa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo,na kuelezea namna Jumia ilivyodhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko. Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii KAMPUNI ya Jumia Tanzania inayojishughulisha na huduma za uuzaji na manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa njia mtandao imemtambulisha Zadok Prescott kuwa Mkurugenzi Mkuu wake mpya. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho wake uliofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Prescott alibainisha ni fursa kwake kujiunga na kampuni hiyo. Ambapo amesema Jumia ni kampuni ambayo imedhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko. “Jumia ilianzishwa mnamo mwaka 2012 ikiwa na imani thabiti ya kwamba: ‘Mtandao wa intaneti unaweza kuboresha maisha ya Waafrika.’ "Ni vigumu kupata bidhaa unayoihitaji kupitia mfumo wa sasa wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali Tanzania. " Upatikanaji wa bidhaa katika sehemu tofauti huwalazimu wateja kusafiri umbali mrefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kuongezea, bei hutofautiana kwa kila mfanyabiashara jambo linalosababisha kuwa ni changamoto kutambua kama unauziwa bidhaa kwa bei sahihi au la,"amesema. Ameongeza ni mfumo ambao humpotezea mteja muda na gharama katika maisha yake ya kila siku. Hivyo dhumuni kubwa la Jumia ni kuufanyia mabadiliko mfumo huo na kuufanya uwe wenye tija kwa wafanyabiashara nchini na kuwapatia wigo zaidi,” alisema Prescott. Akifafanua namna Jumia ilivyodhamiria kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara nchini ameelezea wafanyabiashara wanakumbwa na changamoto lukuki katika uendeshaji wa biashara zao. Ametaja baadhi yake ni gharama kubwa za pango hususani kwenye maeneo yenye wateja wengi. "Hali hii husababisha wafanyabiashara wengi kuwa na idadi ya wateja walewale kulingana na eneo walilopo,” amesema na kuongezea, “Ili kuwafikia wateja kuwajulisha kuhusu biashara zao, inamlamzimu mfanyabiashara kufanya matangazo na kutafuta masoko, jambo ambalo ni gharama kubwa na sio wote wanakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.” Amefafanua Jumia ndio suluhu pekee kwa wateja na wafanyabiashara kwani imekusanya bidhaa za aina tofauti sehemu moja, ikitoa bei zenye ushindani, pamoja na kumfikishia mteja popote alipo kwa urahisi. Amesema mteja anaweza kufanya manunuzi mwenyewe kwa kuingia kwenye mtandao wao, akachagua bidhaa azipendazo na kisha akapelekewe mpaka alipo baada ya kuagiza. " Katika kujenga uaminifu kwa wateja wetu, malipo hufanyika baada ya kumfikia mteja. Kwa kuongezea, mteja huwa hadaiwi malipo pindi asiporidhika na bidhaa aliyopelekewa au akitaka ifanyiwe mabadiliko. "Hivyo, tunawaahidi wateja wetu bidhaa nyingi zaidi kukidhi mahitaji yao, bei zenye ushindani zaidi na kuwafikishia bidhaa popote walipo kwa haraka, urahisi na gharama nafuu,” ameongezea. Amesema zaidi ya kampuni 50,000 za kiafrika zinauza bidhaa zake kupitia Jumia kila siku na kwamba wanafanya jitihada za kuhamisha shughuli za kiuchumi kwenda mtandaoni Na kuziwezesha kampuni za Kiafrika ndogo, za kati na kubwa kupata wateja wapya na kuwahudumia kwa mbinu mpya. " Takribani wajasiriamali na wafanyabiashara 50,000 wanauza bidhaa zao kupitia Jumia, zaidi ya bidhaa 10,000 zinajitangaza kupitia Jumia. "Pia kampuni kadhaa za usafirishaji husafirishaji mamilioni ya bidhaa kila mwaka kwa sababu ya Jumia. Kila siku, tunasaidia na kuhamasisha migahawa, hoteli, wafanyabiashara wadogo, bidhaa, mawakala wa makazi na usafiri, "Makampuni makubwa, kampuni za usafirishaji kuwa bora na kubwa, kwa kutumia msaada wa ripoti za tafiti mbalimbali kuzisaidia kuwa bora na kutoa huduma nzuri kwa wateja," amesema . Ameongeza wanaamini kupitia hivyo wataleta mabadiliko chanya barani Afrika. Prescott amesema mojawapo ya fursa ambayo wafanyabiashara wengi wa kitanzania bado hawajaigundua ni namna ya kuwafikia wateja wanaopatikana mtandaoni. Ambapo amesema ni kwa kujiunga na Jumia, watawapatia fursa ya kukuunganisha na mamilioni ya wateja waliopo mtandaoni. " Tunaweza kumuwezesha mfanyabiashara mdogo anayefanya shughuli zake kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam kuuza bidhaa zake kwa wateja walioko Tanzania nzima. "Tunazitangaza bidhaa tofauti kwa kuziwezesha kuonekana kwa mtu yeyote aliyeunganishwa na mtandao wa intaneti,” amesema. Mkurugenzi Mkuu huyo mpya wa Jumia nchini Tanzania,amesema “wafanyabiashara wanaojiunga nasi hawana haja ya kugharamia shughuli za kutafuta masoko au kukodisha maduka kwa gharama kubwa. "Hii ni huduma ambayo Jumia huitoa kwa kamisheni nafuu kupitia mauzo yatakayofanyika mtandaoni. Kitu pekee tunachokihitaji kutoka kwao ni kuuza bidhaa zenye ubora na bei nafuu kwa wateja wetu.” Katika jitihada za kujenga hamasa ya biashara mtandaoni, Jumia huandaa shughuli za mara kwa mara za kimasoko ndani ya mwaka kama vile kuzindua bidhaa mpya, ofa kabambe na mapunguzo lukuki kwa ajili ya wateja. Kwa upande wake Mkuu wa Masoko wa Jumia Tanzania, Albany James alipata fursa ya kugusia juu ya Jumia kuzindua kwa mara ya kwanza ‘Wiki ya Simu,’ kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Tigo. Ameelezea kampeni hiyo inafanana na kampeni yao ya kila mwaka ya ‘Black Friday,’ lakini hiyo itajikita kwenye bidhaa za simu za mkononi pekee. "Kampeni hii itahusisha uzinduzi wa bidhaa mpya, ofa kabambe, zawadi na punguzo kwa wateja. Tukio hili tayari limekwishafanyika kwenye nchi za Kenya na Nigeria ambapo ni kubwa na maarufu, na kwa mara ya kwanza watanzania watanufaika na mapunguzo ya kuvutia na promosheni zitakazoletwa kwa ajili yao na Jumia. "Itakuwa ni wiki ya aina yake kwa ajili ya kununua bidhaa za simu.Wiki ya Simu’ itaanza Machi 19 mpaka Machi 25 mwaka huu ambapo itazinduliwa kwa muda wa siku mbili, Machi 17 & 18 katika viwanja vya Leaders Club," amesema. Ameongeza uzinduzi huo utazileta pamoja kampuni mbalimbali maarufu za simu nchini katika tukio ambalo litakuwa ni la kipekee, la kifamilia, ambapo wahudhuriaji watakuwa na mazingira mazuri ya kununua bidhaa za simu na kufurahia chakula na muziki mzuri kwa ajili yao. "Tukio hili litawapatia wateja fursa ya kununua na kujionea matoleo mapya ya bidhaa za simu ambazo zinatawala soko kwa sasa kwa gharama nafuu pamoja na kujifunza mambo mengi zaidi kuhusu Jumia,” ameelezea James. Akijaribu kufafanua kwa kifupi kuhusu bidhaa na ofa zitakazokuwepo kwenye ‘Wiki ya Simu,’ Mkuu huyo wa Masoko amesema Jumia kwa kushirikiana na Tigo, zimekuwa ndiyo kampuni za kwanza kuwapatia wateja fursa ya kuagiza simu ya Samsung S9 na S9+ kabla haijaingia sokoni. " Mchakato wa kuagiza Samsung S9 lilianza mara moja kupitia Jumia mara baada ya hafla ya uzinduzi wa simu hiyo kufanyika kwa njia ya mtandao duniani kote kutoka kwenye Mkutano wa Dunia wa Simu za mkononi uliofanyika jijini Barcelona, Hispania Februari 25 mwaka huu. “Wateja watakaoagiza kupitia mtandao wa Jumia wataweza kujipatia simu zao wiki moja kabla ya Wiki ya kampeni, na watapokea kifaa cha kuchaji kwa haraka kinachotumia waya na miezi 6 ya bure ya kuunganishwa na intaneti kutoka Tigo,"amesema. Amefafanua vilevile watakuwa na zawadi za kushtukiza siku ya tukio, katika wiki hiyo wateja wao watapatiwa ‘chemsha bongo’ ya kuitafuta simu ya Samsung S9 yenye thamani ya zaidi ya milioni 2, Amesena ambayo itakuwa imefichwa kwenye mtandao wao kwa kununua bidhaa zenye gharama isiyopungua Sh. 100,000 " Mteja wa kwanza kuivumbua ataweza kujipatia simu hiyo kwa gharama nafuu zaidi nchini. Tutakuwa na ofa za kuvutia, vocha na mapunguzo ambavyo vitawekwa wazi kadri tutakavyokaribia uzinduzi wa wiki hiyo,” amesema James. Kabla ya kujiunga na Jumia Tanzania, Zadok Prescott alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Millicom (kampuni mama ya Tigo na Zantel) katika kitengo cha Kutafuta na Kuunganishaji biashara mpya kuanzia mwaka 2014 mpaka 2018. Prescott anao uzoefu mkubwa katika masuala ya ushauri wa mikakati, utafutaji na uunganishaji wa biashara mpya, kuboresha biashara, ambapo uzoefu wake unatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kupelekea Jumia kuwa mojawapo ya kampuni inayoongoza kwenye utoaji wa za huduma za biashara mtandaoni nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla. Posted by MICHUZI BLOG at Thursday, March 01, 2018 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest DK MWAJELWA AWAPONGEZA WAKULIMA WA CHAI NA PARACHICHI MKOA WA NJOMBE NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akisalimiana na sehemu ya wakulima wa chai alipowasili kwenye kijiji cha Lwangu Wilaya ya njombe mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Ruth Msafiri. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) Sehemu ya wakulima wa chai wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipozungumza nao. Sehemu ya wakulima wa chai wakikusanya zao hilo baada ya kutoka kuvuna wakati Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipofanya ziara na kuzungumza nao. NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea na wakulima wa chai alipotembelea kijiji cha Lwangu Mkoa wa Njombe hivi karibuni. Sehemu ya wakulima wa chai wakimpongeza Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipofanya nao mazungumzo wakati wa ziara yake kwa wakulima hao. Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa akimwagiza Meneja Mkuu wa Njombe Outgrowers Services Company (NOSC), Fibert Kavia (kushoto) kuhakikisha risiti zao zinaonyesha kiasi cha fedha mkulima wa chai anachotakiwa kulipwa baada ya kupima bidhaa hiyo wakati kuuza zao hilo kwa kampuni hiyo. Wanaosikiliza (wa pili kushoto) ni Mkulima wa chai iliyopimwa, Juliana Casian na Karani wa NOSC, Flora Sanga. Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa (wa pili kushoto) akiangali kitalu cha mbegu za kupandikizwa za maparachichi alipofanya ziara na kuzungumza na wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Nundu, Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe. Kushoto ni Afisa Kilimo wa Wakulima wa zao hilo, Damasi Kasalala, Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo na ujumbe wa viongozi wa serikali. Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa akipata maelezo ya mche uliopandikizwa wa parachichi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga (kulia) na Afisa Kilimo, Damasi Kasalala alipofanya ziara na kuzungumza nao wakulima wa zao hilo. Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo. Wataalamu wa kuandaa mbegu za parachichi, Henry Mwepel (kulia), na Lugano Mwalusi wakifanya upandikizaji wa miche ya parachichi kutoka ule wa asili kuwa wa kisasa katika kitalu maalumu cha uzalishali wa zao. NAIBU Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akilakiwa na wakulima wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe mkoani Njombe, alipowatembelea na kuzungumza nao kujua changamoto zao na kutoa ushauri wake kukabiliana nazo. Pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Ruth Msafiri. Wakulima wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe mkoani Njombe, wakimpokea kwa furaha Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa. Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa akiwasabahi wakulima wa viazi mviringo (Irish potatoes) kwenye kijiji cha Lusitu, Wilaya ya Njombe mkoani Njombe alifanya ziara mkoani humo. Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (kulia) Mbunge wa jimbo la Njombe, Mhe. Edward Mwalongo (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga wakifuatilia jambo Mhe. Mwanjelwa alipozungumza na wakulima hao. Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kukusanya, kuchambua, kufungasha na kuuzia viazi mviringo kijiji cha Lusitu, namna bora ya uzalishaji wa viazi wakati Mhe. Mwanjelwa alipofanya ziara na kufanya nao mazungumzo. Posted by MICHUZI BLOG at Thursday, March 01, 2018 No comments: Links to this post Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Older Posts Home Subscribe to: Posts (Atom)

 Mkurugenzi Mkuu mpya wa KAMPUNI  ya Jumia Tanzania,Zadok Prescott akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,alipokuwa akijitambulisha na kueleza mikakati mipya ya kuiendelea kampuni hiyo amayo kwa sasa imezidi kutanuka kila kukicha,kushoto kwake ni Meneja Masoko Albanny Jamess
Meneja Masoko wa Jumia Tanzania, Albanny Jamess akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,kuhusu ujio wa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo,na kuelezea namna Jumia ilivyodhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.

KAMPUNI  ya Jumia Tanzania  inayojishughulisha na huduma za uuzaji na manunuzi ya bidhaa mbalimbali kwa njia mtandao imemtambulisha Zadok Prescott kuwa Mkurugenzi Mkuu wake mpya.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho wake uliofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Prescott alibainisha ni fursa kwake kujiunga na kampuni hiyo.

Ambapo amesema Jumia ni kampuni ambayo imedhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni hususani kwenye soko ambalo bidhaa zipo mbali na wateja pamoja na gharama kubwa za kufanya shughuli za masoko.

“Jumia ilianzishwa mnamo mwaka 2012 ikiwa na imani thabiti ya kwamba: ‘Mtandao wa intaneti unaweza kuboresha maisha ya Waafrika.’  "Ni vigumu kupata bidhaa unayoihitaji kupitia mfumo wa sasa wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali Tanzania.

" Upatikanaji wa bidhaa katika sehemu tofauti huwalazimu wateja kusafiri umbali mrefu kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kuongezea, bei hutofautiana kwa kila mfanyabiashara jambo linalosababisha kuwa ni changamoto kutambua kama unauziwa bidhaa kwa bei sahihi au la,"amesema.

Ameongeza ni  mfumo ambao humpotezea mteja muda na gharama katika maisha yake ya kila siku. Hivyo dhumuni kubwa la Jumia ni kuufanyia mabadiliko mfumo huo na kuufanya uwe wenye tija kwa wafanyabiashara nchini na kuwapatia wigo zaidi,” alisema Prescott.

Akifafanua namna Jumia ilivyodhamiria kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara nchini ameelezea wafanyabiashara wanakumbwa na changamoto lukuki katika uendeshaji wa biashara zao.

Ametaja baadhi yake ni  gharama kubwa za pango hususani kwenye maeneo yenye wateja wengi. "Hali hii husababisha wafanyabiashara wengi kuwa na idadi ya wateja walewale kulingana na eneo walilopo,” amesema na kuongezea,

“Ili kuwafikia wateja kuwajulisha kuhusu biashara zao, inamlamzimu mfanyabiashara kufanya matangazo na kutafuta masoko, jambo ambalo ni gharama kubwa na sio wote wanakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.”

Amefafanua Jumia ndio suluhu pekee kwa wateja na wafanyabiashara kwani imekusanya bidhaa za aina tofauti sehemu moja, ikitoa bei zenye ushindani, pamoja na kumfikishia mteja popote alipo kwa urahisi.

Amesema mteja anaweza kufanya manunuzi mwenyewe kwa kuingia kwenye mtandao wao, akachagua bidhaa azipendazo na kisha akapelekewe mpaka alipo baada ya kuagiza.

" Katika kujenga uaminifu kwa wateja wetu, malipo hufanyika baada ya kumfikia mteja. Kwa kuongezea, mteja huwa hadaiwi malipo pindi asiporidhika na bidhaa aliyopelekewa au akitaka ifanyiwe mabadiliko.

"Hivyo, tunawaahidi wateja wetu bidhaa nyingi zaidi kukidhi mahitaji yao, bei zenye ushindani zaidi na kuwafikishia bidhaa popote walipo kwa haraka, urahisi na gharama nafuu,” ameongezea.

Amesema zaidi ya kampuni 50,000 za kiafrika zinauza bidhaa zake kupitia Jumia kila siku na kwamba wanafanya jitihada za kuhamisha shughuli za kiuchumi kwenda mtandaoni

Na kuziwezesha kampuni za Kiafrika ndogo, za kati na kubwa kupata wateja wapya na kuwahudumia kwa mbinu mpya.

" Takribani wajasiriamali na wafanyabiashara 50,000 wanauza bidhaa zao kupitia Jumia, zaidi ya bidhaa 10,000 zinajitangaza kupitia Jumia.

"Pia kampuni kadhaa za usafirishaji husafirishaji mamilioni ya bidhaa kila mwaka kwa sababu ya Jumia. Kila siku, tunasaidia na kuhamasisha migahawa, hoteli, wafanyabiashara wadogo, bidhaa, mawakala wa makazi na usafiri,

"Makampuni makubwa, kampuni za usafirishaji kuwa bora na kubwa, kwa kutumia msaada wa ripoti za tafiti mbalimbali kuzisaidia kuwa bora na kutoa huduma nzuri kwa wateja," amesema .

Ameongeza wanaamini  kupitia hivyo wataleta mabadiliko chanya barani Afrika.

Prescott amesema mojawapo ya fursa ambayo wafanyabiashara wengi wa kitanzania bado hawajaigundua ni namna ya kuwafikia wateja wanaopatikana mtandaoni.

Ambapo amesema ni kwa kujiunga na Jumia, watawapatia fursa ya kukuunganisha na mamilioni ya wateja waliopo mtandaoni.

" Tunaweza kumuwezesha mfanyabiashara mdogo anayefanya shughuli zake kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam kuuza bidhaa zake kwa wateja walioko Tanzania nzima.

"Tunazitangaza bidhaa tofauti kwa kuziwezesha kuonekana kwa mtu yeyote aliyeunganishwa na mtandao wa intaneti,” amesema.

 Mkurugenzi Mkuu huyo mpya wa Jumia nchini Tanzania,amesema  “wafanyabiashara wanaojiunga nasi hawana haja ya kugharamia shughuli za kutafuta masoko au kukodisha maduka kwa gharama kubwa.

"Hii ni huduma ambayo Jumia huitoa kwa kamisheni nafuu kupitia mauzo yatakayofanyika mtandaoni. Kitu pekee tunachokihitaji kutoka kwao ni kuuza bidhaa zenye ubora na bei nafuu kwa wateja wetu.”

Katika jitihada za kujenga hamasa ya biashara mtandaoni, Jumia huandaa shughuli za mara kwa mara za kimasoko ndani ya mwaka kama vile kuzindua bidhaa mpya, ofa kabambe na mapunguzo lukuki kwa ajili ya wateja.

Kwa upande wake Mkuu wa Masoko wa Jumia Tanzania, Albany James alipata fursa ya kugusia juu ya Jumia kuzindua kwa mara ya kwanza ‘Wiki ya Simu,’ kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Tigo.

 Ameelezea kampeni hiyo inafanana na kampeni yao ya kila mwaka ya ‘Black Friday,’ lakini hiyo itajikita kwenye bidhaa za simu za mkononi pekee.

"Kampeni hii itahusisha uzinduzi wa bidhaa mpya, ofa kabambe, zawadi na punguzo kwa wateja. Tukio hili tayari limekwishafanyika kwenye nchi za Kenya na Nigeria ambapo ni kubwa na maarufu, na kwa mara ya kwanza watanzania watanufaika na mapunguzo ya kuvutia na promosheni zitakazoletwa kwa ajili yao na Jumia.

"Itakuwa ni wiki ya aina yake kwa ajili ya kununua bidhaa za simu.Wiki ya Simu’ itaanza Machi 19 mpaka Machi 25 mwaka huu ambapo itazinduliwa kwa muda wa siku mbili, Machi 17 & 18 katika viwanja vya Leaders Club," amesema.

Ameongeza uzinduzi huo utazileta pamoja kampuni mbalimbali maarufu za simu nchini katika tukio ambalo litakuwa ni la kipekee, la kifamilia, ambapo wahudhuriaji watakuwa na mazingira mazuri ya kununua bidhaa za simu na kufurahia chakula na muziki mzuri kwa ajili yao.

"Tukio hili litawapatia wateja fursa ya kununua na kujionea matoleo mapya ya bidhaa za simu ambazo zinatawala soko kwa sasa kwa gharama nafuu pamoja na kujifunza mambo mengi zaidi kuhusu Jumia,” ameelezea James.

Akijaribu kufafanua kwa kifupi kuhusu bidhaa na ofa zitakazokuwepo kwenye ‘Wiki ya Simu,’ Mkuu huyo wa Masoko amesema Jumia kwa kushirikiana na Tigo, zimekuwa ndiyo kampuni za kwanza kuwapatia wateja fursa ya kuagiza simu ya Samsung S9 na S9+ kabla haijaingia sokoni.

" Mchakato wa kuagiza Samsung S9 lilianza mara moja kupitia Jumia mara baada ya hafla ya uzinduzi wa simu hiyo kufanyika kwa njia ya mtandao duniani kote kutoka kwenye Mkutano wa Dunia wa Simu za mkononi uliofanyika jijini Barcelona, Hispania Februari 25  mwaka huu.

“Wateja watakaoagiza kupitia mtandao wa Jumia wataweza kujipatia simu zao wiki moja kabla ya Wiki ya kampeni, na watapokea kifaa cha kuchaji kwa haraka kinachotumia waya na miezi 6 ya bure ya kuunganishwa na intaneti kutoka Tigo,"amesema.

Amefafanua vilevile watakuwa na zawadi za kushtukiza siku ya tukio, katika wiki hiyo wateja wao watapatiwa ‘chemsha bongo’ ya kuitafuta simu ya Samsung S9 yenye thamani ya zaidi ya milioni 2, Amesena ambayo itakuwa imefichwa kwenye mtandao wao kwa kununua bidhaa zenye gharama isiyopungua Sh. 100,000

" Mteja wa kwanza kuivumbua ataweza kujipatia simu hiyo kwa gharama nafuu zaidi nchini. Tutakuwa na ofa za kuvutia, vocha na mapunguzo ambavyo vitawekwa wazi kadri tutakavyokaribia uzinduzi wa wiki hiyo,” amesema James. 

Kabla ya kujiunga na Jumia Tanzania, Zadok Prescott alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Millicom (kampuni mama ya Tigo na Zantel) katika kitengo cha Kutafuta na Kuunganishaji biashara mpya kuanzia mwaka 2014 mpaka 2018.

 Prescott anao uzoefu mkubwa katika masuala ya ushauri wa mikakati, utafutaji na uunganishaji wa biashara mpya, kuboresha biashara, ambapo uzoefu wake unatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kupelekea Jumia kuwa mojawapo ya kampuni inayoongoza kwenye utoaji wa za huduma za biashara mtandaoni nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment