SERIKALI
imepeleka sh. bilioni 1.92 katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba
wilayani Mtwara kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya.
Hayo
yalibainika jana (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa alipozungumza na wakazi wa Halmashauri hiyo, wakati wa ziara
yake.Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi alisema
fedha hizo zilitolewa na Serikali ili kuimarisha upatikanaji wa huduma
za afya kwa wananchi.
Alisema
jumla ya sh. bilioni 1.2 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha
afya cha kwenye Kata ya Njengwa, ambapo aliwasisitiza watendaji
kutobadilisha matumizi.Waziri Mkuu alisema ujenzi huo utahusisha chumba
cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, jengo la mama na mtoto
na wodi ya wanawake na wanaume, eneo la kuchomea taka na chumba cha
kuhifhadhia maiti.
“Serikali
imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya
afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi
yao.”Aidha, Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao kuendelea kuiunga mkono
Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata
maendeleo.
Pia
Waziri Mkuu alisema Serikali inatarajia kuipitia upya sheria ya elimu
pamoja na sheria ya mtoto ili kuweka masharti ya kumlinda mtoto wa kike
hususani kudhibiti mimba kwa wanafunzi.Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,
Bw. Gelasius Byakanwa alisema Serikali itawachukulia hatua watu wote
watakaobainika kuwapa watoto wa kike dawa za uzazi wa mpango ili
kuwazuia wasipate mimba.
Bw.
Byakanwa alisema wanafunzi wa kike katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba
wamebainika kuwa wanatumia dawa za kuzuia mimba wakiwa shuleni, hivyo
kuwaruhusu kushiriki katika matendo yasiyokuwa ya kimasomo.Alisema
Serikali itafanya msako wa kuwatafuta wote wanaotumia dawa hizo pamoja
na wanaowapa na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa
sababu jambo ni hatari kwa maendeleo ya wanafunzi hao.
Naye,
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Josephat Kakunda alisema
alisema Serikali imepeleka sh. bilioni 1.92 katika Halmashauri ya Mji
wa Nanyamba ili kuboresha huduma za afya.Asema kati yake sh. milioni 700
zilipelekwa katika kituo cha afya cha Nanyamba ambapo sh. milioni 300
zilitumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa na sh milioni 400 ukarabati wa
kituo, huku sh. bilioni 1.2 ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya
Njengwa.
Haya
hivyo, Waziri huyo alisema kuwa Serikali inampango wa kuifanyia
marekebisho sheria ya mtoto kwa kuondoa kipengele cha dhamana kwa watu
watakaotuhumiwa kuwapa mimba watoto wa shule.Alisema hatua hiyo
inatokana na baadhi ya watuhumiwa hao wanapopewa dhamana kwenda
kuzungumza na wazazi au walezi wa binti jambo linalochangia katika
kuharibu ushahidi.” Ni bora wakakaa rumande hadi hukumu itakapotolewa na
kama hawatokutwa na hatia watarudi uraiani”.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MACHI 01, 2018.
No comments:
Post a Comment