Je Mama wa Watoto nane anayegombea kiti cha Urais DRC atafanikiwa? - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 19 December 2018

Je Mama wa Watoto nane anayegombea kiti cha Urais DRC atafanikiwa?

Zimebaki siku nne kwa raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kumchagua mtu atakayerithi mikoba ya Joseph Kabila.
Wagombea watatu ndio wanaotajwa zaidi na ni vigumu hata kudhani kuwa wanaowania kiti hicho wapo zaidi ya ishirini na mmoja wao ni mwanamke.
Bi Marie-Josee Ifoku yupo kwenye kinyang’anyiro cha kurithi Ikulu ya Kinshasa kutoka kwa Kabila akichuana na Emmanuel Ramazani, Martin Fayulu na Felix Tshisekedi ambao ndio wanaouvuma zaidi.
Bi Ifoku, mwenye miaka 53 ni mama wa watoto nane si mgeni katika siasa. Alishawahi kuwa naibu gavana wa jimbo la Tshuapa kwa miezi sita mwaka 2016 kabla ya kuchaguliwa kuwa gavana wa jimbo hilo kuanzia Oktoba 2016 mpaka Oktoba 2017.
Mwandishi wa BBC Swahili Mbelechi Msochi amefanya mahojiano na bi Ifoku hivi karibuni na amemueleza mipango yake endapo Wakongomani watampa ridhaa ya kuwaongoza.
Bi Ifoku anasema kipaumbele chake cha kwanza kitakuwa kufanya mabadiliko ya katiba ili kuhakikisha haki za kiraia zinalindwa na njia ya maendeleo inaandaliwa.
“…kwanza kuwe na mabadiliko kwa upande wa jeshi, polisi pia na uongozi wa kisheria. Tunataka majaji wafanye kazi bila shinikizo, hali itakayowafanya wawekezaji waje wakijua wamehakikishiwa udumishaji wa sheria.”
Ifoku Marie-Josée Mputa Mpunga/Facebook
Bi Ifoku (wapili kulia) anasema kipaumbele chake cha kwanza kitakuwa kufanya mabadiliko ya katiba
Tatizo la vita limekuwa donda ndugu nchini DRC na bi Ikofu amesema atatumia uwezo wake wote kulishughulikia: “Nataka kuwahakikishia raia wa Congo kuwa mwanamke akichaguliwa kama rais tutahakikisha matatizo kama vita ubakaji na mengineyo yatamalizika. Nitazungumza na nchi jirani juu ya namna gani tutaleta amani.”

Nguvu ya wanawake

“Ukiangalia kwa umakini mazingira ya Congo ninaamini kuwa wanawake tupo tayari. Nipo tayari kuiongoza nchi hii. Unajua wanawake wengi siku hizi ni wafanyabiashara na ndio wanaozilisha jamii zao? Wakati mwengine unakuwa ndio mama na baba kwa familia yako. Ni mila na utamaduni tu ndio unaokanganya,” amesema bi Ifoku.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here