Sumaye awaanika maadui wa Chadema - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Wednesday, 19 December 2018

Sumaye awaanika maadui wa Chadema

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)wametajwa kuwa ni maadui ambao watapelekea  chama hicho kukosa ushindi katika chaguzi mbili zijazo.
Akifungua mkutano wa ndani wa Baraza la uongozi la CHADEMA Kanda ya Pwani, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema kuwa, maadui wa chama hicho ni baadhi ya wanachama wanaoweka maslahi binafsi mbele kuliko ya Chama na ya wananchi wanaofifisha jitihada za kukijenga.
Umefika wakati kwa wanachama wetu kufikiria masilahi mapana ya wananchi na chama la sivyo itakuwa vigumu kushika dola, na kama wanachama watajikita kutetea masilahi binafsi kama ilivyotokea kwa baadhi, ni dhahiri lengo la kuongoza nchi halitafikiwa“, amesema Sumaye.
Sunaye ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho baadhi ya wabunge, madiwani, wenyeviti wa halmashauri na wanachama wakijiuzulu nafasi zao na kutimkia CCM ambako baadhi yao walipitishwa na kurudi kwenye nyadhifa hizo.
Uchaguzi wa serikali za mitaa nchini unatarajiwa kufanyika mwakani kabla ya uchaguzi mkuu 2020.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here